CCM:Hatuna historia ya kushindwa uchaguzi zb
Ma Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kutokana na udhaifu wa upinzani ,ukikabiliwa na ombwe la uongozi, hauwezi kukishinda CCM chenye sera za kimaendeleo .
CCM kimesisistiza kushinda baada ya kutekeleza vyema ahadi zake za kisera huku kikihimiza Amani, Umoja na Upendo .
Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Itkadi,Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamisi, aliyesema upinzani unapodai utashinda ni sawa na kuota ndoto mchana .
Mbeto alisema kwa utelelezaji mkubwa wa sera ambazo zimeleta mabadiliko ya maendeleo Zanzibar, hakuna mwananchi atakae upigia kura upinzani.
Alisema ikiwa viongozi wa ACT Wazalendo wanaamini watashinda, matumaini hayo ni sawa na kuisubiri treni ya SGR katika kituo cha daladala .
Mbeto alisema CCM kitapata ushindi kutokana na mageuzi ya kimaendeleo yaliofanyika na baada ya kuwahimiza wanachama wake kujiandikisha katika Dafrari la Kudumu la Wapiga kura.
Mwenezi huyo alisema hata ASP hakikuwa na historia ya kushindwa kwani chaguzi zote tatu za mwaka 1957,1961 na 1963 , ASP kilishinda ila wakoloni hawakutoa madaraka.
Mbeto alisema hata CCM kimendelea kushinda toka mwaka 1995 hadi 2020 na sasa kinajiandaa tena kushinda na kuunda dola .
'Tutashinda kwa kufuata misingi ya demokrasia. CCM ni chama kinachotegemea uamuzi wa walio wengi . Tumemsimamisha mgombea urais anayetakiwa na wananchi, mchapakazi na kiongozi mzalendo ' Alisisitiza.
Hata hivyo Mbeto aliwahimiza wananchi, wafuasi ,wakereketwa na mwnachama wa CCM, kujitoeza ili kujindikishaji wakati utakapowadia.

Post a Comment