CCM:ACT ikimsimamisha Othman ushindi bila jasho Zbar


 Na Mwandishi  Maalum , Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi  kimeihakikishia dunia kuwa ikiwa mgombea  urais wa  Zanzibar kwa tiketi  ya ACT  Wazalendo atasimamishwa Mwenyekiti  wake,  Masoud Othman Masoud, CCM kitashinda bila  kutoka jasho jingi.

Kimewaahidi wazanzibari  ifikapo oktoba mwaka huu ,CCM kitashinda kwa   zaidi  ya kura asilimia 80.2  kuliko  wakati wowote katika historia ya chaguzi kuu za Zanzibar  .

Ahadi hiyo imetolewa na  Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC Zanzibar  Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo ,Khamis  Mbeto  Khamisi  , kufuatia matamshi  ya Othman aliyedai zama ya CCM kiutawala  Zanzibar  itafikia ukomo mwaka huu.

Othman ndiye  Makamo  wa kwanza  wa Rais   chini  ya serikali  ya umoja  wa kitaifa Zanzibar (SUK( toka chama cha ACT  Wazalendo .

Mbeto  akitoa mfano alisema ikiwa fisi anaposhindwa kuutafuna mfupa ngumu mbugani  ,hakuna  mategemeo ya mfupa huo kutafunwa au kuvunjwa paa ambaye  hana meno yenye nguvu wala uwezo  kung'ata vitu  vigumu .

Alisema kama kweli  ACT  Wazalendo  kitamsimamisha Othman na kudhani atamshinda Rais wa Zanzibar  Dk Huseein  Ali Mwinyi ambaye  amefanya mageuzi makubwa ya kimaendeleo ,CCM kitashinda mapema kabla ya saa 5 asubuhi  .

"Tusiandikie mate ilhali wino ungalipo.Hayati  Maalim seif sharif Hamad ambaye alikuwa  gwiji  wa siasa ,na tambo za kudai atashinda kuliko hakukiweza CCM  . Alishindwa toka 1995 hadi 2020 hivyo  kwa  sasa ACT hakina   mgombea mwenye ubavu wa  kuitingisha CCM " Alisema Mbeto 

Aidha Katibu  huyo Mwenezi ameshangazwa na matamshi yaliotamkwa na Waziri  wa Afya SMZ,  Nassor Ahmed  Mazrui,  aliyedai  Zanzibar  inakabiliwa na maisha magumu  huku kudai kuna watu  hupata maradhi kwa kukosa shibe.

'Mazrui  ni Waziri  toka  ACT  aliyewahi kusifu hadharani  maendeleo yalioletwa na serikali  ya Rais  Dk  Mwinyi . Itawashangaza wananchi kumsikia Mazrui  akitoa maneno ya kubeza maendeleo .Hapo ndipo itakapodhihirisha viongozi wa ACT  wamebobea kwa  unafiki wa kisiasa ' Alisema 

Hata hivyo Mbeto  alisema vyovyote  itakavyokuwa madai ya kusema Zanzibar  haijapiga hatua za  maendeleo  wakati   huduma za jamii   zikiimarika ,wananchi hawatakubali  kufungwa vitambaa machoni  mwao iwe hawaoni  yaliofanywa na serikali .

"Viongozi wa ACT punguzeni uongo acheni  wananchi wenyewe waseme.Wana macho yanayoona kila kitu  kilichofanyika. Nyinyi mnapochukua jukumu la kuwasemea  na kuwavunjia heshima .Wananchi  wataendelea kuwadharau kwa kuwaongopea  wakati  wanaona " Alieleza Mbeto 

Katibu  huyo  Mwenezi  alisema  kama ni mabadiliko  ya maendeleo , wananchi wanashuhudia yaliofanyika katika sekta za afya, elimu ,utalii, miundombinu, ajira ,ujenzi  wa vituo vya afya, hospitali, masoko na barabara  Unguja na pemba .

"Othman  na wenzako  acheni siasa  za uongo na kuwafanya wananchi  hawajitambui. Yaliofanywa na Serikali ya Rais Dk Mwinyi yanaonekana. Hakuna mwananachi atakayewamini  viongozi waongo wakati kila kilichofanywa na SMZ  kinaoonekana "Alieleza

Powered by Blogger.