YAS NA TAASISI YA APPS AND GIRLS: WAPIGA MSASA WANAFUNZI WA SAYANSI KUHUSU MASOMO YA TEHAMA

Wanafunzi wa shule ya sekondariI ya Mt Theresa, ya jijini dar es salaam, wameishukuru,Taasisi ya App and Girls kwa kushirikiana na kampuni ya maswalino ya Yas Tanzania kwa kuendesha mafunzo ya TEHAMA kupitia somo la sayansi ili kuwaongezea ujuzi na maarifa katika mafunzo Yao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Carolyne Ekyarisiima, alisema mpango huo unalenga kuondoa tofauti ya kijinsia katika masomo ya sayansi na kuwajengea wasichana uwezo wa kujiajiri.

"Tunatoa mafunzo haya kuanzia ngazi ya shule za sekondari hadi kwa wale walio nje ya mfumo rasmi wa elimu.

ikiwemo Wanajifunza kutengeneza roboti, kuelewa akili mnemba, na kupata ujuzi wa ujasiriamali," alisema Carolyne.

Aidha Yas na App Girls wameendesha programu  hiyo, maalum ya mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi wa sekondari kutoka shule tisa ambazo zinawanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi.

Naye, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Maria mtenga kwa kwa niaba ya wenziwe amesishukuru Yas kwa Kuwapa mafunzo hayo ambayo amesema Kwa hakika yatakuwa chachu na kuleta tija kwenye masomo ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano yaani (TEHAMA).

Mafunzo hayo, nisehemu  ya Kuunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa mstari WA mbele Kuunga mkono Sekta ya Elimu hususani masomo ya sayansi kwa wanawake hapa Nchini.

yanalenga kuwainua wasichana kwa kuwapatia ujuzi wa vitendo katika masomo ya sayansi na ubunifu wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).



Powered by Blogger.