YAS NA MIXX BY YAS: ZAAHIDI KUENDELEA KUUNGA MKONO WAKULIMA NCHINI KUPITIA AMCOS BIL. 110 ZATENGWA

Na. Jumanne Magazi 


6.12.2024

Kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya YAS Tanzania,kupitia kitengo cha Mixx by Yas, imeahidi kuendelea kushirikiana na wakulima kupitia vyama vyao ikiwemo AMCOS.

Akizungumza kwenye hafla maalum mapema Leo 6 Desem 2024 jijini Dodoma Afisa Mkuu wa Mixx by Yas Angelica Pesha

Amesema Kwa miaka saba, "tumekuwa tukiwahudumia wakulima kupitia AMCOS, kuhakikisha malipo ya mazao yao yanafanyika kwa usalama na ufanisi kupitia mfumo wetu wa kidijitali.

Aidha asema Hadi sasa, Mixx by Yas imesaidia kusambaza zaidi ya Tsh 110 bilioni kwa wakulima mbali wa mazao kama Korosho,ufuta,choroko na pamba kupitia AMCOS zaidi ya 500+ kote nchini.

Pesha ameongeza kuwa,Hii ni zaidi ya huduma za kifedha, ni dhamira yetu ya kusaidia wakulima kufanikisha ndoto zao na kuongeza uzalishaji.

Vilevile Pesha amesema Kampeni hii mpaka sasa imeweza kuwazawadia wakulima zaidi ya 90 zawadi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na pesa taslimu, pembejeo za kilimo, na vifaa vya kisasa kama fridge,piki piki,tv n.k. 

"Tukaona tusiishie hapo,tuendele kumpa mkulima wa kitanzania huduma za ziada na nikiri ya kwamba Leo, tunapozindua huduma mpya za kifedha kwa wakulima inayojulikana kana KilimoPesa, tunaipa nguvu  zaidi dhamira hii kwa kuzindua,Mikopo nafuu ya muda mfupi na mrefu – Mikopo hii imeundwa kwa kuzingatia msimu wa kilimo, ili wakulima waweze kukopa na kulipa baada ya mavuno, bila kua na shinikizo la kifedha wakati wa msimu wa kupanda"

Kampeni hizi zimeonesha kuwa tunathamini na kuwatia moyo wakulima kuchagua Mixx by Yas kama mshirika wao wa kifedha wa kudumu.

Aidha Pesha amemalizia kwa kusema pia "tunaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita chini ya Raisi wetu Dr Samia Suluhu Hassan inayosisitiza juu ya umuhimu wa wananchi wote kuwa na Bima ya afya. 

Na kwa kuunga mkono juhudi za wakulima huku tukizingatia afya zao, leo pia mara baada ya uzinduzi huu tutatoa bima za afya zipatazo kumi bure kwa wakulima kumi bora kutoka kanda mabli mbali nchini ambao wameku washirika wetu wa muda mrefu katika kupokea malipo ya mazao ya kupitia Mixx by Yas".



 

Powered by Blogger.