MHE. SILLO AWAPONGEZA WAZAZI BABATI KWA KUTAMBUA UMUHIMU WA ELIMU.
Naibu Waziri Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo amewapongeza Wazazi wa Babati kwa kutambua umuhimu wa elimu ktk kuikomboa jamii na kuhakikisha Watoto wao wanapata elimu bora.
Mhe SIillo ameeleza hayo kwenye mahafali ya wanafunzi wa awali ktk S/M ya mchepuo wa Kiingereza ya Sabnia sambamba na uzinduzi wa shule hiyo iliyopo Kata ya Galapo wilaya ya Babati Des 4, 2024
Mhe Sillo alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa sekta binafsi katika kuboresha elimu hivyo imejenga mazingira wezeshi na rahisi kwa wawekezaji katika sekta ya elimu
Aidha Mhe. Sillo amesema kuwa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ktk kuendelea kuboresha mazingira mazuri ya elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati imejenga zaidi ya madarasa 180 Pamoja na kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo Kituo cha Polisi Galapo na kituo cha Afya cha kisasa kinachojengwa kata ya Galapo. Aidha aliwataka wananchi kuendelea kuunga mkono ilani ya (CCM)
Post a Comment