SERIKALI YAIPA KONGOLE KAMPUNI YA CRJE IKIAHIDI KUENDELEA KUDUMISHA MAHUSIANO MEMA NA CHINA

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imeipongeza Kampuni ya ukandarasi kutoka nchini China ya CRJE (East Africa) Ltd kwa ufanyaji kazi uliotukuka huku ikiahidi kuendelea kukuza mahusiano yaliyodumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania na China Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria Dk Damas Ndumbaro wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Uwajibikaji kwa Jamii ya CRJE kwa ushirikiano na Hoteli ya Johari Rotana.

Hafla hiyo ilihudhuliwa na wageni mbalimbali akiwemo, John Mnali, Mkurugenzi wa Ukuzaji Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mwenyekiti wa Mwalimu Nyerere Foundation Joseph Butiku na balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Ndumbaro, ofisa mwandamizi katika wizara hiyo Shoma Philip Ndono, alisema Kampuni ya CRJE imeongeza kwa kiasi kikubwa uhusiano mwema wa urafiki kati ya China na Tanzania.

 "Tunashukuru na tunatamani urafiki wetu uendelee kudumu kwa muda mrefu ujao.”Alisema kampuni hiyo ya ukandarasi kutoka China ipo Tanzania kwa zaidi ya miaka 55 na imefanya kazi nzuri kwa ustawi wa jamii ya Watanzania.

"CRJE wamehafanya miradi zaidi ya 200 na wametoa mchango mkubwa katika kutoa ajira kwa watanzania pamoja na utekelezaji wa uwajibikaji kwa jamii" alisema



 

Powered by Blogger.