MSALAKA: ARIDHISHWA NA UJENZI WA SKULI TUMBATU

Na. Mwandishi wetu 

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini 'A', Unguja, Bw. Rashid Simai Msaraka amesema ameridhishwa na maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Skuli ya Tumbatu.

Akizungumza wakati akikagua maendeleo ya mradi huo huko Wilaya Ndogo ya Tumbatu, Bw. Msaraka ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo umefikia katika hatua nzuri hivyo amewataka Wasimamizi kuzidisha bidii ili waukamilishe Kwa wakati uliopangwa.

Akizungumzia kuhusu miradi mingine inayojengwa katika kisiwa hicho,Bw. Msaraka amesema ujenzi wa miradi ya barabara na afya tayari umeanza, huku mradi wa bandari na uwanja wa mpira unatarajiwa kutekelezwa baada ya muda mfupi.

Naye Mhandisi Msaidizi katika ujenzi wa skuli hiyo, John Simon, amesema kumekuwa na changamoto katika usafirishaji wa vifaa vya ujenzi kutokana na mazingira ya kisiwa hicho kinachotegemea usafiri wa baharini.

Hata hivyo, amebainisha kuwa wamefanya jitihada kubwa kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.

Mradi wa ujenzi wa skuli ya Tumbatu unatarajiwa kufunguliwa Disemba 31 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, katika shamrashamra za Sherehe za Mapinduzi Zanzibar.
 

Powered by Blogger.