PONDEZA: ACHANGIA MIL 5 UJENZI CHUO CHA VIJANA ZANZIBAR.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Mhe. Ussi Salum Pondeza amechangia shilingi milioni 5 ujenzi wa Chuo cha Umoja wa Vijana Zanzibar.
Ussi amesema ni jambo zuri kuona vijana wanajitoa kwenye utegemeze na kuwa wajasiriamali na kubuni njia za kuwaletea maendelea na sio ya mmoja mmoja bali iwe kwa vikundi vya vijana na kuwasadia vijana wenzao kutoka mitaani na kujishughulisha na kazi za Kilimo na Ufugaji.
"Nakupongeza sana Naibu katibu mkuu UVCCM ZANZIBAR kwa kazi kubwa unayo ifanya katika Jumuiya hii ya Vijana apa zanzibar, Hichi ambacho kimefanyika hapa ndio malengo yetu ya chama cha Mapinduzi Nampongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia pamoja na Dkt. Mwinyi kwa kazi kubwa wanazo zifanya Na sisi Kama wabunge lazima tuwaunge mkono viongozi wetu hawa kwa kazi kubwa wanazo zifanya” amesema Ussi
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa UVCCM Zanzibar Komred Abdi Mahoud Abdi amemshukuru mbunge huyo kwa kuonyesha moyo wa kuwajali na kudhamini Umoja huo wa Vijana Zanzibar na kuwaomba watu wenye uwezo wa kuwasaidia ili kukamilisha miradi yao ya kilimo na Ufugaji.
Post a Comment