NOELI ,NA SAUDA MWINYIMKUU, WAIBUKA WASHINDI WA MIL 1 MAGIFT YA KUGIFT, WIKI YA 6 KUTOKA: YAS, NA MIXX BY YAS
Na. Jumanne Magazi
Kampuni ya Mawasiliano ya Yas Tanzania Leo hii Desemba 20, 2024, imekabidhi zawadi kwa washindi wa 8 PROMOSHENI ya "Magift Kugift 2024.
Balozi wa "Magift ya Kugift" Kutoka Yas Haji Sunday manara akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washindi mbalimbali wa zawadi hizo kwa wiki ya 6 sasa.
Kampuni ya YAS Tanzania imekuwa Ikiendesha promosheni hiyo, kwa muda WA wiki 12 ambapo hadi kufikia Leo zaidi ya kiasi cha Shilingi Zaidi ya mil. 178 zimeshatolewa zikienda kwa washindi mbalimbali sambamba na zawadi hizo zikiwemo simu za mkononi.
Kwa upande wake mmoja wa washindi wa milioni Moja 1 wa wiki hii Noel Digula Digula amesishukuru Yas kwa kuchezesha kampeni hiyo kwani imekuwa ikisaidia kuwapatia zawadi wateja wake ikiwemo pesa taslimu na zawadi nyingine.Naye Bi Sauda mwinyimkuu amesema yeye ameibuka mshindi na hatimaye kipigiwa simu baada ya kufanya miamala mara kwa mara jambo lililopelekea kuibuka mshindi hivyo amewataka watanzania wengine kutumia mtandao wa Yas Tanzania kwani ni mtandao wenye huduma Bora na piaPROMOSHENI ya Magift ya Kugift ni ya ukweli na uwazi na kuwa kila mtu anaweza kushida.
Kwa upande wake Meneja wa Wateja maalum kutoka Mixx by Yas, Mary Lutha amewapongeza washindi WA Magift ya Kugift WA wiki hii ya sita ambapo ametumia hafla hiyo kuwataka wateja wengine WA Mixx by Yas pamoja na Yas Tanzania kuendelea kushiriki Promoshe hiyo kwani kila mmoja ana fursa ya kujishinda zawadi hizo.
Post a Comment