MIXX BY YAS: YALIPA WAKULIMA WA HEWA MKAA,
17.12.2024
Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Yas Tanzania,limetangaza kuingia makubaliano ya ushirikiano na Karagwe Development & Relief Services), KADERE.
Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mkuu wa Mixx by Yas, Angelica Pesha alisema:
“Mixx by Yas tunatambua nafasi muhimu ya teknolojia na huduma za kifedha katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii.
Ushirikiano huu na KADERE unakubaliana na haja ya kimataifa ya suluhisho endelevu za kilimo, kama ilivyosisitizwa katika mkutano wa COP28, na dhamira yetu ya kuleta athari endelevu.
Aidha amesema,Ushirikiano huu unalenga kuboresha maisha ya wakulima wadogo wa kahawa katika wilaya za Karagwe na Kyerwa kupitia mbinu jumuishi zinazozingatia mnepo wa hali ya hewa, ujumuishaji wa kifedha, na kilimo endelevu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa KADERE, Bw. Leonard Kachebonaho, alieleza furaha yake kuhusu ushirikiano huo, akisema:
“KADERE daima imejikita katika maendeleo ya jamii, na ushirikiano wetu na Mixx by Yas ni hatua kubwa kuelekea kutimiza maono yetu ya ukuaji endelevu vijijini. Kwa kushirikiana, tunawawezesha wakulima wa kahawa kiuchumi huku tukihamasisha utunzaji wa mazingira kupitia misitu shirikishi.
Kwa kushirikiana, tunawawezesha wakulima wa kahawa kiuchumi huku tukihamasisha utunzaji wa mazingira kupitia misitu shirikishi.
Ushirikiano huu unaonyesha nguvu ya mshikamano katika kuleta mabadiliko chanya, na tunafurahia athari chanya zitakazotokana na mradi huu kwa maisha ya wakulima wa Kagera na Kyerwa.”
Mixx by Yas imekuwa ikiunga mkono miradi mbalimbali ya wakulima, ikirahisisha malipo na huduma za ugani wa kidijitali kupitia jukwaa la Tigo Kilimo.
Mixx by Yas imekuwa ikiunga mkono miradi mbalimbali ya wakulima, ikirahisisha malipo na huduma za ugani wa kidijitali kupitia jukwaa la Tigo Kilimo.
Ushirikiano wake na vyama vya ushirika zaidi ya 400 vya wakulima, mashirika ya kilimo, na Shirika la Biashara la Serikali ya Zanzibar umeleta mafanikio makubwa, huku zaidi ya TZS bilioni 100 zikisambazwa kwa wakulima zaidi ya 50,000 kote Tanzania Bara na Zanzibar.
Post a Comment