WANAFUNZI 72 SHULE ZA MSINGI KILIMANJARO WAPATIWA MABEGI YA SHULE


Na Jumanne Magazi

Desemba 30, 2024

Kilimanjaro.

Kundi la waendesha baiskeli wapatao 8 wamekamilisha safari ya siku (4)Kutoka mji mkuu wa Kenya Nairobi hadi Kilimanjaro Nchini Tanzania, wakiwa na mabegi (72) yaliyotengenezwa na waendesha baiskeli hao, yenye chapa ya Shirika la ndege la ufaransa la Air France-KLM billboard canvases. 

Akipokea msaada mkoani Kilimanjaro, Meneja mkaazi na utawala Kanda ya Kilimanjaro wa Air France-KLM, Bw Rajat Kumar, amesema mikoba hiyo 72 yenye chapa ya Air France KLM,ikiwa na vifaa mbalimbali vya shule,ikiwemo vitabu na madaftari kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi.

Amesema mikoba hiyo itagaiwa kwa walengwa ambao ni wanafunzi wanasoma shule zote za msingi mkoani Kilimanjaro, hii ikiwa sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamiii  wakati shirika Hilo likianza safari zake Kutoka Ufaransa kuja Kilimanjaro Nchini Tanzania.

" Hizi ni jitihada zinazoonyeshwa na shirika la ndege la Air France-KLM’s

Ambalo limeonyesha nia na nguvu kusaidia juhudi kwenye Elimu hususani kwa maeneo yanayozunguka mkoa wa Kilimanjaro ili kuhakikisha Inahimarika."

Taasisi  ya eco-friendly,imeahidi kuwa  itahakikisha inasaidia wanafunzi  wanafunzi msaada huo ili kutimiza lengo lao la msingi, ambapo kupitia mabegi hayo ambayo ni maalum na ni imara kwa kuwa yemetengenezwa kwa kitambaa cha turubai yanadumu kwa Mazingira ya mikoa ya Kilimanjaro.

Katika hatua nyingine Ranjit amesema wao kama sehemu ya Watoa huduma kwa jamiii wameona hiyo ndio njia sahihi ya kuwekeza kwenye akili ya mwanafunzi ambapo atakumbuka chapa ya Air France KLM, kila atakapobeba Mkoba huo na hiyo ndo shabaha Yao kubwa kuweka urithi kwa ajili ya vizazi na vizazi kupitia Elimu amesema Ranjit"

Kwa upande wao. Waendesha baiskeli hao ambao ndio waliotengeneza mikoba na vifaa hivyo Wamesema malighafii zilizotumika kutengeneza vifaa hivyo ni sahihi kusaidia  Mazingira ya maeneo husika amesema  mmoja wa waendesha baiskeli hao.

"Ambapo amesema mbalimbali na mambo mengine ujio na msaada huo ni kusaidia wanafunzi wote wasio jiweza na wenye mahitaji maalum'.

Tanzania imekuwa nchi ya pili barani Afrika kupokea msaada wa mikoba ya shule 72 kwa wanafunzi shule za msingi, kwa shule zote za mkoa Kilamanjaro ,Kutoka  kwa wahisani shule ya msingi ya Muthangari ya Nchini Kenya eco-friendly school.



Powered by Blogger.