TIGO YAZINDUA,MJASIRIAMALI BOX ILIYOBORESHWA

Na. JUMANNE MAGAZI 

Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo Tanzania, Leo hii Nov 14,2024 imezindua toleo jipya na lililoboreshwa ya Mjasiriamali Box, kifurushi maalum kinacholenga kusaidia Wajasiriamali na Biashara Ndogo ndogo na za Kati (SMEs) kote nchini.

Aidha kampeni hii ya Mjasiriamali Box 2.0 inakuja na huduma mpya na zana muhimu kwa ajili ya kurahisisha shughuli za biashara, usimamizi wa fedha, na kusaidia ukuaji wa biashara katika ulimwengu wa kidigitali.

Akizungumza katika uzinduzi huo,Afisa Mkuu wa Tigo Business, , John Scilima, amesema Mjasiriamali Box inawapa wajasiriamali na SMEs kifurushi chenye router za 5G kwa ajili ya mtandao wa kasi, jukwaa la Usimamizi wa Fedha kwa ufuatiliaji wa mapato na matumizi, pamoja na Portal ya Mjasiriamali Box inayounganisha huduma zote kwa urahisi mahali pamoja.

“Biashara nyingi ndogo ndogo zinapata changamoto ya kupata huduma tofauti kwa ajili ya mtandao, huduma za kifedha, na mawasiliano.

Schilima Ameongeza kuwa Mjasiriamali Box iliyoboreshwa pia inajumuisha mikopo ya biashara kuanzia TZS 120,000 hadi TZS milioni 2, ili kuwasaidia wajasiriamali wanaotaka kuongeza mteja wa biashara zao au kutimiza mahitaji yao ya kila siku. 

Vile vile Kupitia Portal ya Mjasiriamali Box, wamiliki wa biashara wanaweza kuona maendeleo yao na kusimamia shughuli zao zote kwa urahisi.”

Kwa bei ya kuanzia TZS 120,000, Mjasiriamali Box 2.0 ni suluhisho nafuu linaloweza kutumiwa na biashara za aina zote. 

Tigo inaendelea kuonyesha dhamira yake ya kukuza biashara za Tanzania na kuleta ubunifu kwenye sekta ya biashara.



 

Powered by Blogger.