DAUDI EUGENE WA SALASALA: AIBUKA KIDEDEA PROMOSHENI TIGO "MAGIFTI KUGIFT"MIL 5

Na. Jumanne Magazi 

Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo Tanzania Leo hii Novemba 15 2024, imekabidhi zawadi kwa washindi wa PROMOSHENI ya "Magift Kugift"

Akizungumza kwenye hafla ya kuwakabidhi washindi hao zawadi zao, Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema;

“Kama ilivyo kawaida yetu, Tigo tunapenda kuweka furaha kwenye nyuso za wateja wetu, hivyo basi tumekuja tena na kampeni iitwayo Magift ya Kugift ambapo wiki hii tumefanya droo ya kwanza ya kutafuta washindi na tumepata jumla ya washindi 42, waliojishindia simu janja, washindi saba waliojishindia shilingi milioni moja kila mmoja na mshindi mmoja amejishindia shilingi milioni tano.

Mmoja wa Washindi  wa Promosheni hiyo Mfanyabiashar Daud Eugene mkaazi wa salasala jijini dar es salaam, ambaye  ni mshindi Kutoka kundi la Wafanyabiashara kutoka Dar es Salaam

Akieleza jinsi wateja hao walivyojishindia zawadi hizo, Mary alisema walichofanya ni kufanya miamala mbalimbali kwa kutumia Tigo Pesa.

Amesema kwa wafanyabiashara wao walijishindia zawadi hizo kwa kupokea malipo ya bidhaa wanazouza kutumia huduma Lipa kwa simu ya Tigo kutoka mitandao mbalimbali.

Ameishukuru Tigo kwa kuendesha Promosheni hiyo na amewataka watanzania kuendelea kujitokeza kushiriki Promosheni pamoja na huduma zinazotolewa na kampuni hiyo kwani ni bora na za uhakika.

Kwa upande wa Wateja washindi wa shilingi milioni moja waliofika kwenye hafla hiyo kuchukua zawadi zao ni Adrian Milandu, Issa Masoud, Saadie Mwinyi, Zena Chiputa na Hilda Mavaga.   


 

Powered by Blogger.