TIGO: YAJA NA "MAGIFTI KUGIFTI" KUELEKEA MSIMU WA SIKU KUU ZA MWISHO WA MWAKA

Na. Jumanne Magazi 
7.11.2024

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Tanzania Leo hii imezindua msimu mpya wa siku kuu za mwisho WA mwaka “Magifti ya Kugifti” yenye lengo la kusherehekea miaka 30 ya kuungana na wateja, mawakala, na wafanyabiashara wake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Angelica Pesha, amesema Katika kipindi chote cha kampeni ya Magifti ya Kugifti, wateja wa Tigo wana nafasi nyingi za kushinda zawadi za kuvutia. 

Aidha ameendelea kusema kuwa Kila siku, wateja wanaweza kujishindia hadi TSh milioni 1 pamoja na simu janja sita kila siku—jumla ya simu 540 zitakazotolewa katika kampeni hii.

Pesha, amesisitiza umuhimu wa kuthamini wateja  kwa kusema, “Kwetu sisi kutoka Tigo Pesa, wateja wetu ndio msingi wa kila kitu tunachofanya. Magifti ya Kugifti ni shukrani zetu za dhati kwa kila mmoja wao. 

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Isack Nchunda, ameonesha furaha yake kuhusu msimu huu wa kutoa na kutafakari safari ya Tigo kwa miaka 30 iliyopita. 

Amesema Mwaka huu umekuwa wa kipekee,kwa kunipitia ubunifu, niseme tu shukrani kwa imani ambayo wateja wetu wanayo kwetu. 
Aidha amesisitiza kuwa Kupitia Magifti ya Kugifti, tunasherehekea miaka 30 ya kuungana na wateja wetu na kuwashukuru kwa zawadi zinazowaleta karibu na kuinua jamii nzima.”

Nchunda ameelezea jinsia ya kushiriki kampeni hiyo ambapo amesema wateja wanachotakiwa kufanya ni kufanya miamala ya Tigo Pesa au kununua vifurushi vya sauti kupitia njia yoyote ili kujiunga na kujishindia zawadi hizi kem kem Mawakala na wafanyabiashara(Lipa Kwa Simu) wanaweza kushiriki kwa kufikia viwango maalum vya miamala, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya Tigo kusaidia ukuaji wa wadau wake.

“Magifti ya Kugifti” inaonesha dhamira ya kampuni ya kuongeza tafrija za mwisho wa mwaka na kuwezesha wateja, mawakala, na wafanyabiashara kumaliza mwaka kwa furaha na kuanza 2025 kwa matumaini na ari mpya. 

Powered by Blogger.