TANZANIA ZIMBABWE ZAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO YA ULINZI NA UTAALAMU
Na. JUMANNE MAGAZI
7.11.2024
Katika Kuhimarisha uhusiano na ushirikiano Serikali ya Tanzania imeingia Makubaliana ya kushirikiana Katika masuala ya ulinzi na usalama na Zimbabwe ili kuendelea kukuza uhusiano ambao umedumu kwa siku nyingi.
Hafla ya utiaji saini hati za makubaliano hayo yamefanyika leo Nov 7, 2024 jijini Dar es Salaam kupitia Waziri wa Ulinzi Tanzania, Stagomena Taxi na Waziri wa Ulinzi wa Zimbabwe, Oppah Muchinguri.
Waziri Stagomena Tax, akizungumza baada ya shughuli ya utiaji saini na ubadilishaji wa hati hizo kukamilika, amesema mchakato huo unaendelea kuimarisha ushirikiano ambao umedumu tangu wakati wa kupigania Uhuru wa nchi hizo.
"Makubaliano haya ya leo, yanaendelea kudumisha umoja na mshikamano ulioasisiwa na marais wetu, Mwalimu Julius Nyerere na Robert Mugabe wa Zimbabwe," amesema.
Ameongezea kuwa wananchi wa Zimbabwe wanawakumbuka sana hayati, Mwalimu Nyerere na Hashimu Mbita kwa namna walivyohusika katika harakati za ukombozi wa taifa hilo kutoka kwa wakoloni.
Ameongeza kuwa ushirikiano huo utakuwa Katika nyanja mbalimbali ikiwemo kubadilishana teknolojia kwa masuala ya kijeshi, mafunzo na mambo mengi yatakayoimarisha Ulinzi na usalama Katika nchi hizo na kanda ya kusini mwa Afrika.
Waziri Taxi, ameongeza kwamba wameingia kutokana kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kuhamasisha kuendelea kuwepo na ushirikiano na nchi na mbalimbali na kujenga ushiriikiano mzuri.
Hivyo nimshukuru Sana Rais Samia kwa kutaka tuendelee na kujenga mahusiano mazuri na nchi mbalimbali na ndio maana leo tumeingia makubaliano haya na Zimbabwe, amesema Waziri Taxi.
Naye Waziri wa Ulinzi wa Zimbabwe, Muchinguri amesema kwamba anajivunia kuingia makubaliano na Tanzania jambo ambalo linaendeleza ushirikiano wa siku nyingi wa nchi hizo.
"Ushirikiano huu kwetu utaendelea kuimarisha ushirikiano wa siku nyingi ulioasisi na viongozi wetu, Mwalimu Nyerere na Comred Mugabe", amesema.
Baada ya shughuli hiyo kufanyika Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es Salaam kwa pamoja walimbelea Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa( JKT), Mlalakuwa na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika la Uzalishaji Mali.
Pia katika ziara hiyo walimbelea kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa ya Uhuru na kuona utendaji kazi wa kiwanda hicho, pamoja na kupata maelezo kuhusu shughuli zinazofanywa na SUMA JKT.
Post a Comment