TIGO: YAGAWA MISAADA MBALIMBALI KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM DAR
Na Jumanne Magazi
Kampuni ya Mawasiliano, TIGO Tanzania katika kuelekea kufunga mwaka, wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwenye kituo cha sinza maalumu kilichopo jijini dar es salaam chenye watoto zaidi ya 93.
Akizungumiza mara baada ya kutoka msaada huo Mkurugenzi wa Tigo Dar es salaam, Aidan Komba amesema kama TIGO Tanzania wanatambua umuhimu wa watu wenye mahitaji maalumu na kuona kunaulazima wa kurejesha Kwa jamii faida wanayoipata.
Msaada iliyotolewa kituoni hapo ni pamoja na charahani, magodoro, chupa, mahotipoti kwaajili ya kuhudumia jamii hiyo yenye uhitaji maalumu.
Sanjali na hayo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Catherine Msese ametoa shukrani zake Kwa kampuni ya TIGO Tanzania Kwa msaada waliowapatia kwaajili ya shule hiyo
" Kwa kweli msaada huu utawasaudia watoto kujimudu katika kufanya kazi zao za Kila siku kwani tumepata vifaa vya usafi, vitawasaidia watoto katika kufanya usafi hapa shuleni na vifaa vya cherehani vitawasaidia katika mafunzo ya ufundi" alisema
Aidha msese ameitaka jamii kuwa na utaratibu wa kuishi kwa kupendana ikiwemo kuwa karibu na watoto na jamii yenye nahitaji maalum ili kurudisha shukran kwani kwa kufanya hivyo Kuna mpendeza mungu
Post a Comment