MRADI WA UMEME RUSUMO KUZINDULIWA FEBRUARI 2025
Hayo yameelezwa leo Novemba 16, 2024 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kikao cha Mawaziri wa Nchi hizo tatu wanaohusika na usimamizi wa mradi huo.
Ameongeza kuwa, utekelezaji wa mradi wa Rusumo umefikia asilimia 99.9 na upo katika hatua za umaliziaji vitu vidogo vidogo.
"Kukamilika kwa mradi huu unaiwezesha kila Nchi kupata megawati 27 katika gridi yake ya Taifa." Amesema Dkt.Biteko
27 megawati 3,070.
Ameongeza kuwa, mradi wa Rusumo utakuwa kichocheo kikubwa cha uchumi kwa kuiunganisha Tanzania na Nchi za Burundi na Rwanda katika biashara ya umeme.
Amesisitiza kuwa, uwepo wa vyanzo vingi vya kuzalisha umeme utasaidia kukuza uchumi wa Nchi na maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Kuhusu matumizi ya umeme kwa siku nchini amesema asilimia 52 ya umeme inatumiwa na wananchi na asilimia 48 inatumika kwa ajili ya viwanda.
Post a Comment