WAAFRIKA MIL 300 WATAPIKIA NISHATI YA UMEME IFIKAPO 2030: BITEKO
JUMANNE MAGAZI
16.10.2024 Dar es salaam
Naibu Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko amesema ifikapo mwaka 2030 watu million 300 katika Bara la Afrika wawe wamefikiwa na umeme ili watu wengi waweze kutumia nishati safi ya kupikia.
Ameyasema hayo mapema leo hii alipokua katika uzinduzi wa mkutano wa 9 wa siku 2 wa soko la Nishati Afrika ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati uliofanyika jijini Dar es Salaam katika hotel ya Hayyat
Amesema juhudi zinazofanyika katika kufikia lengo hilo zimepelekea Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Benki ya Dunia ( WB) kuunga mkono Ajenda ya Nishati Safi ya kupikia katika bara la Afrika.
Biteko amesema hayo wakati akizungumza katika Mkutano wa Jukwaa la Majadiliano kuhusu Masuala ya Nishati kwa Bara la Afrika kwa ngazi ya Mawaziri unaofanyika Jijini Dar es salaam kwa siku mbili ulioandaliwa na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na AfDB.
Aidha, amesema jambo jengine ni kwamba mkutano huo utakua ni maandalizi ya mkutano wa wakuu wa nchi wa Afrika wanaokwenda kujadili masuala ya nishati kwenye bara la Afrika kwani kuwapata watu 300 sio kazi rahisi kuishia kwenye ngazi ya Wizara.
Ameongeza kuwa, lengo la mkutano huo ni kwenda kujadili na kufanya tafakuri kubwa kama bara juu ya upatikanaji wa Nishati safi ya kupikia ambapo mfumo wake unachangamoto nyingi kwenye utekelezaji wake.
Kwa upande wake, Makamo Mwenyekiti wa Nishati, mabadiliko ya tabia nchi na ukuaji wa kijani AFDB Dr Kevin kairuki wameamua kufanya kazi kwa pamoja na Tanzania kwa sababu ipo mstari wa mbele katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
0 Comments