SERIKALI IPO TAYARI KUONGEZA VYANZO VINGINE VYA NISHATI YA UMEME IKIWEMO JUA NA JOTO ARDHI:KAZUNGU
Akizungumza mara baada ya kuhitimisha Mkutano wa 57 wa Wakurugenzi na maofisa wa ngazi za juu Nishati barani Afrika ambao umefanyika Leo Oktoba 15 2024, jijini Dar es salaam.
Aidha Kazungu amesema Lengo la kikao hiki cha watalaam wa masuala ya umeme kutoka nchi za Jumuiya ya SADC kupanga mikakati ya kuona namna gani wanaweza kutumia umeme kwa pamoja na kushirikiana kupitia nchi hizo zinazounda Jumuiya ya SADC, katika kufua umeme kusafirisha pamoja na kusambaza umeme kwa wateja.
Aidha, amesema wao kama Serikali wanamradi moja unaitwa Taza ambao mradi huo unakuasudia kuunganisha umeme kati ya Tanzania na Zambia pamoja na mambo mengine wanapokutana katika vikao kama hivo wanajaribu kupitia katika hatua walizofikia, changamoto walizonazo ili waweze kujipanga vizuri waweze kuzitatua ndio hasa lengo la mkutano huu.
Kama mahitaji ya umeme kwa Tanzania tupo vizuri, Ile mradi wetu mkubwa wa bwawa la Mwalimu Nyerere unazalisha megawatt 700 ambapo tageti Yao ni kuzalisha megawatt 900 lakini pia ukiachana na bwawa hilo pia tunavyanzo vyengine vya kuzalisha sola kupitia mfumo wa jua tunazalisha megawatt 600 kupitia joto ardhi tunazalisha megawatt 5000.
"Sisi kama Serikali tunahakikisha tunajipanga vizuri kuweza kuzalisha umeme kupitia vyanzo vyengine,ili tuweze kuongeza megawatt katika Taifa letu tuna mradi mpya unaitwa ....ambao unasaidia kuboresha miundombinu ya umeme pia kuzalishaji vyanzo vipya umeme katika Taifa letu na kuunganisha mikoa iliyopo pembezoni kama kigoma na Mtwara, lindi na Katavi"
Mikakati yetu ni kuhakikisha wanaendelea wanafua umeme wa kutosha na wenzantu wa jirani tutakapounganisha miundombinu hii tutafanya biashara nzuri sana ya kuwauzia umeme hasa ukizingitia wenzetu wa Zambia kwa sasa wanachangamoto ya umeme"
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji uzalisahi umeme TANESCO, Mhandisi Costa Rubagumya, amesema Tanzania iko katikati ya ‘East Africa Powe Pool’ ambako inapatikana Kenya na kwa upande wa ‘Southern African Power Pool’ inapatikana Zambia.
“Katika maeneo hayo mawili inatupa uwezekano wa kusaidiana katika nyanja ya umeme ikiwa nchi mojawapo inapokuwa na shida ya nishati hiyo, mfano eneo la Kariba kwa sasa lina ukame na kusababisha Zimbabwe na Zambia kupitia katika kipindi kigumu na kutokana na kuwepo kwa ushirikiano huu unatoa fursa ya kusaidiana na kutuweka salama katika nyanja ya umeme,” amesema.
Post a Comment