SPIKA TULIA AKSON MGENI RASMI TUZO ZA EJAT 2024


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Tulia Akson anataraji kuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha utoaji wa Tuzo za 11 za Umahiri wa Uandishi WA Habari Tanzania (EJAT) Septemba 28, 2024 katika ukumbi Diamond jubilee jijijini Dar es salaam.

Akizungumza kwenye mkutano na  Waandishi wa habari hii Leo. September 19,2024, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya EJAT 2023, Ernest Sungura, ambaye pia ni katibu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), amesema washindani 72 wamethibitishwa kuwania Tuzo hiyo baada ya Kupita mchujo wa kazi 1,135 zilzowasilishwa kwenye kamati ya maandalizi ya EJAT Kutoka Tanzania bara na Visiwani.
Aidha amefafanua kuwa kati ya Waandishi wa habari 72 wanaume ni 45 (sawa na asilimia 62.5%) na wanawake 27 (sawa na asilimia 37.5) kati ya wateule hao wateule 14 (19%) wanatoka katika runinga 13(18%) Wanatoka vyombo vya mtandaoni, radio 20 (28%) na wateule 25 (35%) wanatoka kwenye magazeti., ambapo amesema katika Tuzo hizo ambazo zimegawanywa kwa mshindi wa kwanza WA pili na watatu pamoja na mshindi WA jumla, huku Mgeni Rasmi ndiye atakayekabidhi Tuzo kwa mshindi wa jumla ambaye atakuwa amewapiku wenginie kwa vigezo vilivyowekwa na jopo la majaji.


Aidha amesema kuwa Waandishi wa habari wa mkoa WA Dar es salaam wameongoza kwa kuwasilisha kazi  zipatazo 290 wakifuatiwa na MKOA WA Arusha waliotuma kazi 81 mwanza kazi 74, Iringa ilishika nafasi ya Nje kwa kutuma kaz 72, huku kwa upande wa Zanzibar Kutoka mkoa wa kaskazini Pemba  (36) KUSINI Pemba(43) huku MKOA wa mjini magharibi zilitumwa kazi (29).
Sungura amesema mchakato huo ulianza kwa dirisha la kupokea kazi za Waandishi habari lilifunguliwa tokea Nov 15,mwaka Jana na kufungwa February 28 mwaka huu, huku kazi za kuchambua na kutathmini ubora WA kazi za kihabari za mwaka 2023 ulianza tar 7 hadi 15 mwaka huu.

Jopo la majaji liliongozwa na mwenyekiti HALIMA Shariff,katibu wake akiwa Dkt Egbert Mkono na majaji wengine wakiwa ni. Pamoja na ndugu Mkubwa ally,Eshe muhidini, Jenifer Sumi, na HALIMA Mselemu na Absalom Kibanda.




Powered by Blogger.