MWENYEKITI WA CCM MKOA WA TANGA MH.RAJAB ABDALLAH AMEONGOZA MAMIA YA WANANCHI WA MKOA HUO KUMFANYIA DUA YA KUMREHEM ALLY MOHAMED KIBAO ALIYETEKWA NA KUUAWA HIVI
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga, kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mh. Rajab Abdallah ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, kushirikiana na uongozi wa Msikiti wa Ijumaa, Familia ya Marehem Ally Mohamed Kibao, kimefanya dua maalum ya kumrehemu aliyekuwa kiongozi wa siasa wa Chama Cha upinzani CHADEMA, ambaye alikuwa mwananchi wa Tanga.
Akizungumza baada ya dua hiyo, Mwenyekiti wa CCM Tanga, Mh.Rajab Abdallah ameishukuru familia na wanatanga kwa ujumla kukaa kwa utulivu na mshikamano katika kipindi hicho kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao, Ali Mohamed Kibao, ambaye alizaliwa katika familia ya viongozi wa dini, jambo ambalo limemsukuma kuandaa dua hiyo.
Pia, Mh. Rajab Abdallah, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alitumia adhara hiyo kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kauli yake dhabiti ya kukemea vitendo vya utekaji, uuaji na kuagiza Mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika na mauaji ya Ally Mohamed Kibao.
"Katika hili, tumesikia kauli ya Rais Dk.Samia ya kusikitishwa na tukio hili, kukemea tukio hili na matukio mengine yanayo shabihiana na hili. Tunampongeza Rais Dk.Samia kwa kauli yake ya kukemea vitendo hivyo viovu, ambavyo havipendezi, tunaunga mkono kauli yake ya kutoa maelekezo kwa Mamlaka husika, kuhakikisha uchunguzi wa kina na weledi, kuhakikisha vikundi na wote waliohusika na vijana.
Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Kamati Kuu,l ya CCM, Mh. Rajab Abdallah, amehimiza wananchi wa Tanga na Tanzania kwa ujumla kumwombea Rais Dk.Samia kwa kazi kubwa anayoifanya.
"Tuendelee kumwombea Rais Dk.Samia kwa kazi kubwa anayoifanya, kuongoza nchi sio mchezo ni jambo kubwa, Tuendelea kumwombea Rais Dk.Samia katika uongozi wake kwa jukumu kubwa alilonalo la kuongoza nchi,"amesisitiza.
Vilevile, aliwapongeza wanafamilia ya marehemu Ali Kibao, kwa utulivu na ushirikiano wao kwa kukubali kufanyika dua hiyo huku akiwashukuru wananchi wa Tanga kwa kujitokeza kwa wingi katika Dua hiyo kuunga kuwafariji wanafamilia.
Awali mwakilishi wa familia ya Ali Kibao, Ally Hemed Abeid amesema familia wanatoa shukrani za dhati kwa jumuiya yote ya watu wa Tanga akiwemo Mwenyekiti wa CCM Abdallah kwa kuwashika mkono katika kipindi chote hivyo Mwenyezi Mungu atawalipa.
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Jafari Kubecha, aliwashukuru wananchi wa Tanga, kwa subira zao na utulivu wao katika kipindi chote huku akiwataka kuendelea kudumisha umoja na kuungana na familia hiyo.
Amesema, Mkoa na Wilaya hiyo ni salama na wataendelea kudumisha umoja na usalama na hawataruhusu mtu yeyote kuvuruga amani iliyopo ambapo serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali za dini kuhudumia wananchi.
Post a Comment