BODI YA MUKOPO HESLB,NIDA,RITA WATANGAZA KIAMA WANUFAIKA MIKOPO ELIMU YA JUU

Na. Jumanne Magazi 

11.septemba 2024.

Hatimaye Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu HESLB, Ikishirikiana na Taasisi zingine za Serikali ikiwemo RITA,NIDA, CREDIT INFO, zimetiliana sahihi na kubadirishana hati za makubaliano kufanya kazi kwa pamoja,ili kubaini na kuwafikia wanafunzi wote wasiolipa mikopo waliopewa na bodi ya mikopo Tanzania.

Akizungumza wakati  wakati wa hafla fupi ya kubadirishana hati za ushirikiano kati ya HESLB, na wadau wa Kimkakati, iliyofanyika leo September 11 2024. Jijijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Dkt Bill Kiwia amesema ushirikiano huo ni mkakati wa kuunga Mkono agizo la RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye aliagiza ifikapo December mwaka huu mifumo yote ya Serikali unapaswa kusomana

Kiwia amesema hadi sasa Zaidi ya Shilingi 600 bilioni zinapaswa kurejeshwa lakini hadi hadi sasa wahusika bado hawajaresha.

Vile vile kiwia ameongeza kuwa  Muungano WA Taasisi hizo unaboreshwa kukusanyaji WA mikopo ili kusaidia Serikali kuendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaostahiri kupata mikopo ya Elimu ya juu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa NIDA Deusdedit Bubelwa amesema, NIDA inajukumu kubwa kushirikiana na HESLB ili kurahisisha kuwafikia wadau wake.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Mkuu WA Credit Info Tanzania Edwin Urasa amesema kwa upande wao wako tayari kushirikiana na bodi ya mikopo ili kusaidia urahisi wa mchakato wa utoaji huduma zake ukiwemo mikopo hiyo Nchini.


 Aidha Urasa ameendelea kusema wao wanajukumu KUITUNZA na kukusanya kumbukumbu na taarifa  za Taasisi mbalimbali ikiwemo HESLBL hivyo watajitahidi kufanya kazi kutunza na kubaini wanufaika wote WA mikopo ili kujua taarifa zao kwa ujumla.

Wakati huo huo Mkurugenzi mkuu wa RITA,Fransis Kanyusi anasema wao kama wadau muhimu kwenye Muungano huo wanao wajibu kufanikisha harakati za bodi ya mikopo nchini HESLB ili kuboresha mchakato wa kukusanya mikopo kwa wadaiwa sugu hivyo Muungano huo, unalenga kuunga Mkono juhudi za Serikali katika kukusanya mapato.





Powered by Blogger.