TUNADI SERA NA SIYO CHUKI, UBAGUZI NA UVUNJIFU WA AMANI - DK.MWINYI

Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka  Wanasiasa kunadi sera za kuwaletea wananchi maendeleo na siyo kueneza chuki, ubaguzi , uvunjifu wa amani , pia amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuhubiri amani na iwe kipaumbele chao namba moja katika mikutano ya hadhara na kujibu hoja zote kwa takwimu. 


Dk.Mwinyi aliyasema hayo alipozungumza na Kamati za Siasa za Matawi, Wadi , na Majimbo za Mkoa wa Mjini katika ukumbi wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani tarehe 7 Agosti 2024.

Halikadhalika Dk.Mwinyi amesema suala la mikataba ya  bandari Zanzibar na mamlaka ya viwanja vya ndege  halijabinafishwa , Serikali imeingia mikataba ya uendeshaji

Kwa upande mwingine Dk.Mwinyi amesema Serikali imetekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa asilimia kubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, miundombinu, masoko, viwanda, michezo, ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi  wa Serikali na posho zao , pensheni za jamii kwa Wazee ,Wastaafu nakadhalika .

Makamu Dk.Mwinyi amehimiza umoja , mshikamano kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi , akisisitiza kazi ni moja ushindi wa kishindo kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.

 

Powered by Blogger.