SERIKALI YAIPA HEKO TIArb KUPUNGUZA MIGOGORO YA KIBIASHARA



Na. JUMANNE MAGAZI

Katika kile kinachoonekana  kuridhishwa na Kasi ya  kupungua kwa migogoro na ufumbuzi wa kibiashara .

Serikali imeipongeza Taasisi  ya usuluhishi WA migogoro ya biashara TIArb kwa kuendelea kutatua changamoto nyingi za kibiashara.

SERIKALI imesema inaridhishwa na kasi ya usuluhishi migogoro nchini na kuchangia kupunguza migogoro katika nyanja za uchumi,siasa na kijamii.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Jumanne Sagini,wakati wa Mkutano wa saba wa Taasisi ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (TIArb) uliofanyika Jijini Hapa.
Sagini amesema uzoefu unaonesha usuluhishi wa migogoro nje ya mahakama inasaidia kupunguza nguvu na muda kwenye mashauri Mahakama.

"Watu wanapokutana na watu waliobobea kwenye masuala husika wanapotatua migogoro inachukua muda mfupi na miradi inaweza kuendelea kuliko kwenda mahakamani huko Mahakama inachukua muda mrefu na ndio maana Serikali tunaridhika na Taasisi hizi"Amesema Sagini.

 
Hata hivyo,Sagini,amesema kwa Sasa Serikali imeweka sera za kuanzishwa Taasisi za Usuluhishi Migogoro na mpaka sasa zimefika saba ili kuwasaidia Watanzania au wawekezaji kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo .

Sagini pia ametumia mkutano huo kuzitaka Taasisi za Kusuluhisha Migogoro kuongeza nguvu hasa kipindi hiki ambapo Serikali ya awamu ya sita imefungua milango ya uwekezaji nchini.

Kwa Upande wake Katibu wa 
Taasisi ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (TIArb),Husaje Adam Mwambene,amesema mkutano wa saba ulioanza tangu na jana na unamaliza leo ulikuwa umejikita katika mambo kadhaa ikiwemo masuala kujadili kusuluhisho Migogoro ya Katika sekta ya Ujenzi Kimataifa.

Mwambene amesema lengo Taasisi hiyo imeanzishwa kwa lengo la watu wenye migogoro kusuluhisha nje ya mahakama.
Powered by Blogger.