FCS, CLOUDS, VODACOM, KUJA NA WIKI YA AZAKI SEPT 9 HADI 13 JIJINI ARUSHA

Taasisi ya Foundation civil society  FCS, Imeandaa Wiki ya Asasi za kiraira AZAKI ambayo itafua FCCtiwa na Mkutano mkuu wa  mwaka ambayo itaanza kuanzia Septemba 9 hadi 13 2024, ambayo itafanyika mkoani Arusha Mount Meru.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam hii Leo Mkurugenzi mkaaza wa Civil International Mercia Mahenge amesema wiki ya Azaki hufanyika kila mwaka na huu ni mwaka 6 kwa Azaki kufanya mkutano wao.
Aidha Bi Mahenge amesema wao wakishirikiana na Taasisi ya Ubongo International  ambao ndio washiriki wa wakuu WA maandalizi ya mkutano huo.

Amesema Wiki ya Azaki huandaliwa wa Staring Comit Tanzania "ambapo amesema sisi kazi yetu ni kuangalia Sekta zote ambazo wanashirikiana nazo wakianza na Asasi za kiraia lakini pia wanaanagalia upande wa Serikali kuangalia changamoto ambazo wanakutana nazo.

Vilevile Mkurugenzi huyo mkaazi amesema "wao Taasisi ya Kimataifa wanashirikiana na Wadau wa maendeleo kwa ujumla jinsi gani wanaweza kushirikiana ili kuleta maendeleo Nchini kwetu Tanzania".

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa WA Taasisi ya Tanzania Foundation Civil Society TFCS TFCS,Justice Rutenge ameelezea dhumuni la wiki ya Azaki ambapo amesema lengo kuu ni kuangalia dira nzima ya maendeleo Taifa na ndio maana wameamua kupanua wigo WA ushiriki WA wiki Azaki hivyo amewaomba watanzania wote kushiriki wiki hiyo ya Azaki mjini Arusha.

Rutenge amesema wao katika wiki hii ya Azaki wamekuja na kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni Voice ,Vision Value akimaanisha Sauti dira na thamani.

Aidha amesema moja ya kazi Yao ni kuangalia Dira ya kila mwaka inazungumza Nini ambapo amesema kwa mwaka huu Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa hivyo wao nao wana wajibu wa kuhamasisha jamii kushiriki Uchaguzi huo na ule WA mwakaani.

Katika hatua nyingine amesema dira ya Taifa lolote lile Duniani huendeshwa kwa dira hivyo wao kama Asasi wameamua kuchukua sauti za umma ili kupaza kwa lengo la kufikisha maendeleo yao Serikali ambao ndio watekelezaji WA kuu dira hiyo.

Vile vile Rutenge amefafanua Zaidi mambo yatakayokuwa yakifanywa kwenye wiki hiyo ya Azaki kuwa ni pamoja mjadala mbalimbali Shughuli za kijamii na Makongamano mengi yenye lengo la kukumbusha jamii na Serikali umuhimu wa Asasi za kiraira kwa Leo la maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa Ubongo Mwasi Wilmore amesema kama kampuni ya kitanzania wameamua kushirikiana na FCS katika kuandaa Wiki ya Azaki kwani nao wanawajibu wa kushirikiana ana Serikali katika kufanikisha maelengo Yao hivyo amewaomba Wananchi kufatilia hatua kwa hatua maendeleo ya wiki ya Azaki ambapo kilele chake litakuwa kule mkoani Arusha Mwaka huu.


Powered by Blogger.