WAZIRI MKUU AZINDUA V.A.R MITAMBO MIPYA
Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano WA Tanzania,Kasim Majaaliwa Leo Julai 15 2024 amezindua vifaa vya kisasa vya kurushia matangazo ya televisheni yaani outside broadcasting truck, sambamba na Uzinduzi wa Chanel mpya ya Azam sports 4HD pamoja na mfumo WA mwendo wa mechi za SOKA VAR.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri mkuu Majaaliwa ametumia fursa hiyo kuwapongeza kampuni ya Azam Media kwa uwekezaji wake huo wenye Gharama kubwa.
Awali Mkurugenzi mkuu wa maudhui wa Kampuni ya Azam media ltd ambaye amemuwakilisha Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bakhresa Group Abubakar Bakhresa, Patrick kahemele Ameishukuru Serikali kwa kuendelea kusapoti kampuni ya Azam katika utendaji wake.
Uzinduzi huo ni muendelezo wa uwekezaji mkubwa unaofanywa na Azam media limited katika Miundombinu ya kuongezea ubora WA matangazo ya ligi kuu ya Tanzania NBC Premier league pamoja na michezo mingine.
Aidha katika Kahemele amesema Magari hayo ya kurushia matangazo yana teknnolojia ya kisasa yenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya uzalishaji WA mchezo wowote wa soka kwa uhitaji wa viwango vya Shirikisho la soka Duniani Fifa.
Kuhusu maboresho ya soka Kahemele amesema Azam media wameamua kuongezea Chanel mpya ya Azam sports 4HD, Chanel hii itakuwa ikionyesha michezo yote kwa njia Bora kwa mfumo wa kisasa yaani HD.
Post a Comment