UVCCM YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KILIMO WENYE THAMANI YA ZAIDI YA MIL 140 KUTOKA CHINA


Jumuiya ya vijana ccm UVCCM Leo hii imepokea msaada wa pawatila na mashine ya kukuobolea MPUNGA wenye thamani ya Zaidi  ya Shilingi mil 200,kutoka kwa kampuni ya Guangzhou company limited ya nchini China.

Akizungumza wakati wa kupokea Msaada huo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohamed Kawaida Ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo kwani umekuja kwa wakati muwafaka.

Kwa upande wake Muwakilishi WA kampuni hiyo ambao ndio wadhamini bwana Xinag ji amesema wao wamekuwa mstari WA mbele katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya TANZANIA chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Naye Katibu mkuu wa UVCCM JOKETI Mwegelo amesema vifaa hivyo vimeletwa kwa lengo la kuinua vijana WA kitanzania ambao ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo msaada huo utatumika kama chachu kwa maendeleo ya vijana na  Taifa  kwa ujumla.

 

Powered by Blogger.