TUMUENZI MANDELA KWA VITENDO: SUMAYE
Watanzania na Dunia kwa ujumla wametakiwa kuyaenzi mema yote yaliyofanywa na aliyekuwa Rais wa kwanza Mzalendo wa Afrika kusini hayati Nelson Mandela
Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson.
Rai hiyo imetolewa na aliyekuwa Waziri mkuu wa Awamu ya tatu Mh Fredrick Sumaye wakati wa Kongamano la kumbukumbu ya siku ya Kimataifa ya Mandela iliyofanyika Leo Julai 18, 2024 jijini Dar es salaam.
Sumaye amesema Dunia na wanajamii kwa ujumla wametakiwa kumuenzi kiongozi huyo kwa vitendo.
Aidha Maadhimisho hayo ambayo hufanyika Julai 18 ya kila mwaka siku ya kuzaliwa ya Mandela kama sehemu ya kutambua mchango wake kwa jamii za Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla maalum ya kuadhimisha siku hiyo iliyoandaliwa na taasisi ya Victorious Center for Exellence, Waziri Mkuu msataafu, Frederick Sumaye amesema maisha ya Mandela alikuwa kiongozi mzalendo ambaye maisha yake yameacha alama ambayo kila mtu anapaswa kujifunza.
Sumaye amesema Mandela alikuwa kiongozi ambaye alikuwa muuumini wa demokarisia,usawa, haki na usawa, umoja na ushirikiano pamoja na upendo.
Alitolea mfano baada ya Mandela kutoka jela na kushinda uchaguzi mkuu wa Afrika Kusini na hivyo kuwa rais mpya wa nchi hiyo watu wengi walitarajia angelipiza kisasi kwa makaburu kwa kuwafanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi.
"Mandela hakufanya hivyo ila alihimiza umoja, upendo na demokrasia huku akisisitiza haki sawa kwa watu wa rangi zote katika nchi ya Afrika Kusini"amesema.
Pia ameongeza kuwa Mandela alikuwa kiongozi ambaye alihimiza umoja na ushirikiano na alikuwa tayari kujitolea kuwasaidia wengine
"Maisha ya Mandela yametufundisha na ametuachia mambo mengi, kubwa likiwa ni kusamehe na kuwa tayari kujitolea maisha kwa ajili ya wengine katika dunia hii, pia Mandela ametufundisha kuwa na matumaini ya kile tunachokipigania badala ya kuwa waoga.
Kwa upande wake Mkuu wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Shabnam Mallick amesema Mandela hakuwa kiongozi wa Afrika pekee bali ni dunia nzima.
"Mandela kiongozi wa aina yake na mfano wa kuigwa katika wakati wetu, alipigania utu na usawa na pia kuchagiza ujasiri, wema na alikuwa tayari kujitolea uhuru wake na hata maisha yake kwa ajili ya wengine"amesema.
Naye Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Noluthando Mayende-Malepe amesema maadhimisho hayo ni muhimu kwa ajili ya kutambua jitihada zake katika kutatua migogoro, kukuza na kulinda haki za binadamu, usawa wa jinsia na haki za watoto na makundi mengine yaliyo hatarini; mapambano dhidi ya umaskini.
Post a Comment