KATAVI ITAPATA UMEME WA GRIDI YA TAIFA MWEZI SEPTEMBA MWAKA HUU - DKT. BITEKO
Hatimaye Mkoa wa Katavi unatarajiwa kuingizwa katika matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa ifikapo mwezi Septemba, 2024 baada ya kuikosa huduma hiyo kwa zaidi ya miaka sitini ya Uhuru Tanzanaia.
Hayo yamebainishwa leo Julai 9, 2024 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Doto Biteko baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Njia Kuu ya kusafirisha umeme ya Msongo wa Kilovoti 132, kutoka Tabora hadi Katavi na Kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme kilichoko mkoani Mpanda.
Post a Comment