WAJASILIAMALI BUYUNI: WAMIMINIKA KUJISAJILI MIKOPO YA 10% YA DKT SAMIA
Na Jumanne Magazi
Mwagisa amewataja baadhi ya wafanyabiashara na wajasiliamali ambao wanakwenda kunufaika na mikopo hiyo kuwa ni pamoja na wauza chipsi mama na baba lishe,wauza mboga mboga na wengineo watakao kidhi vigezo vya mikopo huo.
Nao baadhi ya wafanyabiashara na wajasiliamali wa kata ya Buyuni akiwemo Anderson Samweli selenda,na Agness Focus ambao wamejitokeza Kushiriki zoezi hilo la kujisajili wameishukuru Serikali na uongozi wa kata ya Buyuni kuratibu zoezi hilo, ambalo wamesema linakwenda kuwanufaisha wao na familia zao.
10.06.2026
Dar es salaam
Zoezi la uandikishaji na usajili wa wafanyabiashara Wadogowadogo maarufu kama wajasiliamali wa kata ya Buyuni na viunga vyake limefunguliwa rasmi leo, Juni 10,2026.
Aidha Bandia amewaomba wakazi, wafanyabiashara na wajasiliamali wote wa kata ya Buyuni kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo adhwimu ili kupata mikopo hiyo ya Asilimia 10 kama ilivyokusudiwa.
Naye Afisa Maendeleo ya jimii kutoka Halmashahuri ya jiji la Dar es salaam Bi Tatu Mwigasa amesema zoezi hili ni muendelezo wa juhudi za Mh Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, ambaye ameahidi kutoka mikopo hiyo wa wajasiliamali ili kuweza kuwasaidia kimaendeleo.Mwagisa amewataja baadhi ya wafanyabiashara na wajasiliamali ambao wanakwenda kunufaika na mikopo hiyo kuwa ni pamoja na wauza chipsi mama na baba lishe,wauza mboga mboga na wengineo watakao kidhi vigezo vya mikopo huo.
Nao baadhi ya wafanyabiashara na wajasiliamali wa kata ya Buyuni akiwemo Anderson Samweli selenda,na Agness Focus ambao wamejitokeza Kushiriki zoezi hilo la kujisajili wameishukuru Serikali na uongozi wa kata ya Buyuni kuratibu zoezi hilo, ambalo wamesema linakwenda kuwanufaisha wao na familia zao.
Huu ni muendelezo wa juhudi thabiti za Diwani wa Kata ya Buyuni Mh Jesca Mahamoud Msolla, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupambania haki na fursa za wanabuyuni ikiwemo mikopo hii ya Asilimia 10 maarufu mikopo ya Samia.






Post a Comment