SHEIKH SWED TWAIBU: MWENYEKITI MPYA (TMWN) AZOA KURA ZA KISHINDO


 Tanzania Muslim Welfare Network (TMWN) inayojumuisha Taasisi mbalimbali za kidini zilizosajiliwa rasmi Mambo ya ndani iliyoundwa miaka 9 iliyopita kwa lengo la kutengeneza mtandao wa kijamii utakaoungana ili kutengeneza Jimbo (Constituency) litakaloungana na majimbo mengine ya kijamii hapa Tanzania. 

Mapema tarehe 16 Mei 2026 imepata Viongozi wapya katika uchaguzi uliofanyika Ukumbi wa Mtambani, Kinondoni Mjini  jijini Dar es Salaamu. Uchaguzi huo umefanyika kutokana na uongozi uliokuwepo kumaliza muda wake.

Nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa ilichukuliwa na Sheikh Swed Twaibu Swed akimshinda mpinzani wake Alhaji Othman Ntaru (Katibu Mkuu wa BAKWATA mstaafu na Kamishina wa TACAIDS mstaafu). Sheikh Swed anakuwa Mwenyekiti wa awamu ya taru akiwa ametanguliwa na Mwenyekiti anayemaliza muda wake Sheikh Abdushakur Omari  (Mkurugenzi wa Tawala za mikoa na Wilaya BAKWATA) na aliyekuwa  Mwenyekiti wa kwanza Sheikh Issa Othman Issa ( IMAMU Mkuu Masjid Maamour na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Taifa - BAKWATA).

Sheikh Swed Twaibu ni Mwenyekiti Mtendaji wa TCDO, Mratibu ofisi ya Mufti Tanzania na Katibu wa Sekretarieti ya Baraza la Ulamaa Taifa 

Nafasi ya Katibu imechukuliwa na  Mwalimu Juma Sultan akiwa amechaguliwa kwa kipindi kingine cha pili na watangulizi wake ni Alhaji Othman Ntaru na Dr. Pazi Mwinyinvua. Nafasi nyingine ni ya Mwekahazina iliyochukuliwa na Sheikh Salum Mbwana, nae ametanguliwa na Mwekahazina aliyemaliza muda wake Bi Khadijah binti Dr. Ahmed Twaha na kabla yao ni Marehemu Suleimani Lolila aliyewahi kuwa Katibu Mkuu BAKWATA. Wote hawa watahudumu kwa muda wa miaka 3 wakati Mwenyekiti atahudumu kwa muda wa miaka mitano. Mwenyekiti wa Mkutano wa uchaguzi alikuwa Sheikh Ahmad Shebe akisaidiwa na Sheikh Said Mpeta pamoja na ustaadhi Selemani.

Akifunga kikao hicho Mwenyekiti mpya Imamu Swed, aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua kwa kura nyingi na akasema ataomba ushirikiano ili kuendeleza mtandao wetu ambao unaonekana kulegalega ukilinganisha na wakati ule wa mwanzo. Kikao kiliwaagiza viongozi hao kuipitia Katiba ili iendane na hali halisi ya sasa. Alifunga kikao kwa Dua iliyosomwa na Sheikh Mohamed Hariri (mjumbe Tanga) saa 6:10 mchana.

Powered by Blogger.