KAMILISHENI UJENZI VIWANJA VYA MAZOEZI AFCON KABLA YA MWEZI WA 8: RC CHALAMILA
14.05.2026
Dar es salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert John Chalamila amewataka wakandarasi kuongeza Kasi ya ujenzi wa Mradi wa Viwanja maalum vya mazoezi kwa ajili ya Mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika Afcon 2027.
Sambamba na Hilo, Mkuu huyo wa Mkoa amewaomba wananchi wa kinondoni kutumia fursa ya mashindano ya Afcon, kutoka kukuza uchumi wao kwa kufanya biashara mbalimbali zinazozunguka viwanja hivyo.
" Nisem tu ndugu zangu Wana kinondoni fursa hii iliyokuja katika wilaya yetu, nilazima tuitumie kikamilifu katika kujipatia kipato Cha mtu mmoja mmoja au kwa familia kwa ujumla, kupitia michuano hii mikubwa barani Afrika"
Aidha Chalamila amesema kupitia mradi huo serikali imetenga kiasi Cha zaidi ya Bilioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa viwanja hivyo ambapo hadi sasa ujenzi huo umefikia ASILIMIA 23 na bado kazi inaendelea ambapo unataraji Kukamilika mwezi desemba mwaka huu" Amesema Chalamila.Kipekee nimshukuru MH Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa Uzalendo wake na hatimaye kukubali kutofedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya michezo ikiwemo viwanja hivi vya mazoezi vitakavyotumiwa na timu zitakazo kuja kushiriki michuano hiyo
Naye Mkuu wa wilaya ya kinondoni MH Saad Mtambule amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa yeye na timu yake watakuwa wakitembelea mara kwa mara ujenzi huo,ilikuhakikisha unakamilika mapema na haraka.
Awali Diwani wa Kata ya Kinondoni Mh Idrissa Said Ngatiche ameshukuru mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kwa ziara yake hiyo ambapo amesema.
"Kwa upande wetu sisi kama Wana kinondoni tumepokea mradi huu mkubwa na wa kimkakati ambao utaleta maendeleo chanya kwetu sisi kama Wana kinondoni kwa kukuza fursa za kiuchumi kwa vijana wetu" amesema Diwani Ngatiche."Kipekee tuna Mshukuru MH Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kujenga viwanja hivi,ambavyo vina kwenda kutupa fursa mbalimbali za kiuchumi tunaomba tupelekee salamu zetu za shukran kwa Mh Rais" Amesema Diwani Ngatiche.Ikumbukwe nchi za Kenya Uganda na Tanzania zitakuwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa ya soka barani Afrika ambayo imepangwa kufanyika mwaka 2027.











Post a Comment