DIWANI IDRISSA NGATICHE: AZINDUA MGHAHAWA MPYA WA "TEA POINT" KINONDONI
17.05.2026
Dar es salaam
Diwani wa kata ya kinondoni MH Idrissa Ngatiche mapema Leo amezindua mgahawa mpya unaokwenda kwa jina la TEA POINT, uliopo kinondoni jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wageni waalikwa Waliohudhuria, uzinduzi huo, Diwani Ngatiche ameupongeza uongozi wa Mghahawa huo kwa kitendo cha Kufungua kitu muhimu katika kata hiyo.
"Mimi siku zote nimekuwa nikivutiw na kupendezwa na juhudi na maendeleo yanayofanywa na kuanzishwa na wanakinondoni wenzangu, lakini jambo zuri ni kuona kuwa Mghahawa huu umefunguliwa ndani ya kata yangu jambo jema sana na lakufurahisha. Amesema Diwani Idrissa.
Aidha Idrissa amesema umeona kwenye uzinduzi huu watu Wengi ni wanakinondoni na bila shaka Mghahawa huu umekuja sehemu nzuri kwa wanakinondoni wote.
"Ndugu zangu kwenye miaka ya 2004-2005, wakati namaliza shule, kuliwahi kufunguliwa biashara ya chipsi na ndugu yetu anaitwaa Omar mpemba, alikuwa pale mtaa wa Togo kama sikosei alikuwa akijaza sana watu miaka hiyo"
Na mara kadhaa nilikuwa nikienda pale nilikuwa na mkuta Mufti wetu Sheikh Abubakar zubeir Bin Ali wa Mbwana kipindi hicho alikuwa bado hajawa Mufti.
Katika Hafla hiyo ya uzinduzi watu maarufu Waliohudhuria ni pamoja na Sheikh wa wilaya ya Korogwe, Sheikh Ali Zubeir Mbwana, na watu Wengi mashuhuri na wakazi wa kinondoni wakiwemo Viongozi wa chama cha mapinduzi.
Mgahawa upo jirani na (upstairs) ya Car Wash iliyopo mkabala na ukumbi wa PJ Hall (zamani Lang'ata Social Hall, au FM Club) na utakuwa ukitoa huduma hizo kuanzia saa 1:00 asubuhi mpaka saa 3:00 usiku.



Post a Comment