MKURUGENZI DAR: ATAKA UKARABATI SHULE/MSINGI NYEBURU UKAMILIKE HARAKA

Na Jumanne magazi 

18.04.2026

Dar es salaam 

Mkurugenzi wa jiji la dar es salaam Bw.Elihuruma Mabelya, amemtaka Mkandarasi wa ujenzi wa ukarabati wa shule ya ya awali na msingi Nyeburu kukamilika wakati ujenzi wa mradi wa madaraja 5 na matundu 10 ya choo, iliyopo mtaa wa Nyeburu.

Ameyasema hayo hii leo April 18 2026, wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi huo,unaojengwa kwa gharama za fedha za serikali, ambapo amesikitishwa kutokamalika kwa wakati kwa ukarabati huo.
Aidha,Elihuruma amesema hakuna kinafanya ujenzi huo Kwenda polepole wakati fedha za mradi huo zipo na tayari zimeshatolewa na Mkandarasi ameshaanza kazi.

"Nashangaa kuona hadi sasa baadhi ya maeneo hayakamilika ikiwemo matundu ya choo ,sakafu na maeneo mengine ambayo kila kitu kimeshatolewa ugumu unatoka wapi" alihoji mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Omar Mwinchande, ametoa taarifa ya Ripoti ya maendeleo ya ujenzi huo mbele ya mkurugenzi wa jiji ambapo amesema, shule hiyo ilianzishwa rasmi mwaka 2003,na walipokea fedha za mradi mnamo tarehe 22/08/2025 kiasi Cha Shilingi mil 120, kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 5 na matundu 10 ya choo,kutoka kwa mkurugenzi wa jiji la dar es salaam, ambazo ni fedha za mapato ya ndani ilisema sehemu ya taarifa ya hiyo.

Aidha omaar amesema ujenzi huo umeanza rasmi mnamo tarehe18.12.2025,Aidha amezungumzia hali ya mradi hadi sasa madaraja matano (5) yamefikia hatua ya kuskimu, huku matundu 10 ya choo yapo kwenye hatua ya plasta.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Buyuni, MH Jesca Mahmoud msolla ameshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa ahadi zake ambayo ni elimu na tabasamu kwa mtoto wa Tanzania lazima ipokelewe kwa asilimia mia moja.
Vilevile Diwani Jesca ameshukuru Mkurugenzi wa halmashahuri ya jiji la dar es Bw Elihuruma Mabelya, ambaye amesema baada ya kuletewa changamoto ya shule hiyo aliweza kuchukua hatua kwa wakati na hatimaye    kuidhinishwa fedha za kutoka  mfuko wa dharula chini ya Asilimia 10 tayari kwa ukarabati wa shule hiyo.
Naye Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyeburu, Sadati Athumani Rwetabula, amemshukuru mkurugenzi wa halmashahuri ya a jiji kwa msaada mkubwa alioutoa kwa kutenga fedha hizo na pia kuwa mwepesi kila anapompigia simu hakusita kupokea na kusikiliza changamoto yake.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa viongozi wa kata ya Buyuni chini ya Diwani Jesca msolla kuwa karibu na  Wananchi ambapo amewaomba kuwa watu wa matokeo zaidi na kuwasikiliza changamoto zao,kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza Imani kubwa kwao na kazi wanazofanya zitaleta maana 

Mkurugenzi huyo ameahidi kurudi tena baada ya siku 14,ili kujionea maendeleo ya mradi huo huku akiomba wasaidizi wake kutenga muda mwingine ili afanye ziara nyingine kwa ajili ya kutembelea miradi mingine ya maendeleo inayosimamiwa na halmashahuri ya jiji la dar es salaam.








 

Powered by Blogger.