WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA ASHUHUDIA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA NA JESHI LA MAREKANI ZIKISAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO KIJESHI
Dar es salaam
12.03.2026
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dk. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 12 Machi,2026, katika ofisi ndogo za Wizara ya Ulinzi na JKT, Upanga, jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi cha Jimbo la Nebraska nchini Marekani (Nebraska National Guard), Meja Jenerali Craig Strong, aliyeambatana na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini, Mhe. Andrew Lentz, pamoja na maafisa jenerali kadhaa kutoka Nebraska.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya JWTZ na Jeshi la Marekani, Waziri wa Ulinzi na JKT, Mhe Rhimo Nyansaho amelipongeza Jeshi la Ulinzi wa Tanzania na Jeshi la Ulinzi la Marekani la Nebraska kwa kufikia hatua hiyo muhimu ya kihistoria katika sekta ya Diplomasia ya Ulinzi na akamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake yaliyohakikisha makubaliano hayo yanasainiwa na kuanza kutekelezwa.
Waziri wa Ulinzi na JKT akaongeza kwa kusema imeridhishwa na hatua hiyo ambayo inayoakisi na sera ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika kudumisha mahusiano ya kimataifa na akaahidi kuhakikisha makubaliano haya yanatekelezwa kwa faida ya nchi za Tanzania na Marekani na watu wake.










Post a Comment