MIL. 231 KUKAMILISHA ZAHANATI KATA YA KIMANGA: DIWANI LYMO

Na Mwandishi wetu 

25.03.2026

Dar es salaam 

Diwani wa kata ya Tabata Kimanga Mh. Julius Peter Lymo amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa wa Tanzania Dkt.Samaia Suluhu Hassan, kwa fedha za ujenzi wa Zahanati kwenye kata hiyo.

Akizungumza na Peruzi media hii Leo, March25,2026,Lymo amesema serikali kupitia Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam baada ya kuipatia kiasi Cha Shilingi Million 231 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati hiyo, ambayo itakuwa ikitoa huduma mbalimbali ikiwemo jengo la wajawazito, wagonjwa wa nje yaani OPD, na nyinginezo.

Kwa upande wake Fundi mkuu ambaye amezingumza kwa niaba ya Mkandarasi wa ujenzi wa zahanati hiyo Bw Juma Rajabu ameshukuru serikali ya mtaa,mtaa wa Kimanga akiwemo Diwani, Mwenyekiti wa serikali ya mtaa pamoja na kamati nzima ya utekelezaji kwa kuwapatia,zabuni hiyo.
Aidha Rajab amesema kila kitu kina kwenda sawa ikiwemo upatikanaji wa Vifaa,fedha na huduma zote kwa wakati jambo ambalo linapekea kuendeleNa ujenzi huo kwa Kasi huku akiahidi kukabidhi jengo Hilo ndani ya kipindi kilichowekwa kwenye mkataba huo,licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa ikiwemo mvua na mambo mengine ambayo yanaathiri ujenzi huo.

Nao Wakaazi wa kata ya Kimanga Joseph Shayo na Aziza Ali Msigara, kwa pamoja wamemshukuru serikali kwa kuwajengea Zahanati hiyo, ambayo inakwenda kuondoka kero ya huduma ya afya iliyokuwepo kwa muda mrefu 
Zahanati hiyo inatarajiwa Kukamilika ndani ya kipindi cha miezi miwili ijayo ambapo wananchi watakuwa wakipata huduma zote za Afya pindi itakapo kamilika 





 

Powered by Blogger.