MSIOGOPE KUVAA SARE ZA CCM MITAANI: SILE

Na Jumanne magazi 

03.01.2026

Dar es salaam 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ccm, wilaya ya ilala Said Sile, amewaasa wanachama wa CHAMA hicho kuacha kuogopa kuvaa sare za Chama hicho kwani hakuna Cha kuogopa kwani CCM ndio chama tawala na kinashika dola.

Ameyasema leo, January 03 2026, wakati wa mkutano wa Halmashahuri kuu ya kata ya Buyuni,akiwa ndiye Mgeni rasmi mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Maramasha Buyuni nje kidogo ya jiji la dar es salaam.

Sile amesema ni "kweli usiopingila kwa siku za hivi karibuni viongozi na wanachama Cha mapinduzi tumekuwa na hofu ya kuvaa sare au alama zinazotuonyesha kuwa sisi ni wanachama jambo ambalo amesema kwa sasa hatuna haja ya kuogopa  badala yake tujivunie na kuvaa kwa kujiamini " amesema Sile.
Aidha Mwenyekiti huyo pia ametumia mkutano huo, kuwaasa wanachama wa chama hicho kuunga mkono jitihada za viongozi wa ngazi zote kwani ndio viongozi waliochaguliwa na Wana ccm na wananchi na badala yake wawaunge mkono viongozi wao.
Awali Diwani wa kata ya Buyuni Mh Jesca Mahmoud msolla, amemshukuru Mgeni rasmi,na kumuahidi kufanya Kazi kwa bidii kwa kushirikiana na viongozi pamoja na kamati tendaji,ambapo amesema "muda wa kucheka umekwiaha na kwamba viongozi wa mashina,na wenyeviti hawata lala Tena kama yeye halali" hivyo ajiandae kupokea mashtaka kutoka kwao.
Vilevile Mh. Jesca amemuahidi mgeni rasmi kuwa yuko tayari kupokea maelezo ya aina yoyote kutoka kwa viongozi wa juu chama na serikali yenye lengo chanya kwa ajili ya  kuwatumikia wananchi hususani Wana Buyuni  na maeneo mengine kwa ujumla,huku akisisitiza kuwa kwa sasa kazi ndio imeanza rasmi hakuna tena  muda wa maneno kwani yeye sio kiongozi wa maneno amesema diwani huyo.
Katika hatua nyingine   JESCA ametoa rai na kusema kuwa yeye ni kiongozi wa Kata ya Buyuni lakini kiongozi Hana  mipaka amemuahidi mgeni rasmi kuwa yuko tayari kushirikiana na viongozi wa kata zingine,katika kumsaidia Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, ambaye Nia yake nikuwaletea maendeleo wananchi na yeye kama diwani yuko tayari kutimiza Ilani ya chama Cha mapinduzi.

Huu ni mkutano mkuu wa kwanza wa Halmashahuri kuu ya kata ya Buyuni, ambao pia umetumika kama sehemu ya kuwashukuru wanachama hicho kwa kukiwezesha chama Cha mapinduzi kushinda uchaguzi mkuu uliopita, lakini pia mkutano huo umetumika sehemu ya kutoa salamu za mwaka mpya 









 

Powered by Blogger.