WAZIRI WA NISHATI MHE. NDEJEMBI AZINDUA RASMI MITA JANJA
šAelekeza mita hizo kusambazwa katika maeneo yote yenye uhitaji
Waziri wa Nishati amezindua Mita janja hizo Disemba 05, 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wadau wa sekta ya nishati na watendaji wa TANESCO.
“Leo tunajivunia hatua kubwa ya kihistoria zilifanywa na TANESCO ikiwa ni moja ya kampuni za umma inayofanya vizuri katika utoaji huduma kwa wateja nchini. Mita janja inaleta mapinduzi makubwa katika namna Shirika hili linavyofanya usimamizi wa ukusanyaji wa mapato,” ameeleza Mhe. Ndejembi.
Ameongeza kuwa changamoto zilizokuwa zikiwakabili wateja wakati wa kuingiza token ndiyo zimeisukuma Serikali kufanya mageuzi ya kiteknolojia.
“Uzinduzi huu unaweka alama kubwa kwa nchi yetu kwenye mapinduzi ya tekinolojia , hivyo naielekeza TANESCO kuhakikisha inasamabaza mita hizi maeneo yote yenye uhitaji mkuwa na kuhakikisha inaendana na viwango vya kimataifa sambamba na kutoa elimu za faida ya mita hizo,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema uzinduzi wa Mita Janja ni mwendelezo wa dhamira ya Serikali katika kuboresha huduma kwa wananchi.





Post a Comment