TUTAANZISHA CHAMA CHA VIJANA WANAO JITAMBUA KULINDA MAADILI: DIWANI JESCA MSOLLAH

Na Jumanne magazi 

Dar es salaam 

28,Dec 2025

Diwani wa kata ya Buyuni Jesca Mahmoud Msollah amesema anampango wa kuanzisha chama Cha vijana wanaojitambu katika kata hiyo kwa kushirikiana na wenyeviti wa Serikali za Mitaa hiyo ikiwa na lengo la kusimamia dhana ya malezi Bora kwa vijana.
Ameyasema hayo leo desemba 28 2025, jijini Dar es salaam wakati akizindua Tamasha maalum la Dailema Festival 2025,kata ya Buyuni, Chanika nje kidogo ya jiji la dar es salaam.

Amesema katika kuulinda uzalendo na kusimamia tamaduni za kitanzania ameona Kuna haja ya kusaidia juhudi za Mh Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan,ambaye amekuwa mstari wa mbele kulinda maadili na tabia njema kwa vijana wa kitanzania 
Msolla amesema jamii Bora huanza na vijana hivyo katika kulitekeleza hilo, amewaasa wazazi  na walezi kwa ujumla kushirikiana na serikali katika kulea vijana wao kwa lengo la kulinda amani ya nchi jambo ambalo ni tunu ya taifa 

Katika hatua nyingine Diwani huyo,ameahidi kuendeleza michezo katika kata yake ambapo mbali na mambo mengine ameahidi ligi ya kata ambayo itahusisha timi mbalimbali kutoka kata hiyo huku yeye akiahidi kutoa zawadi ya NG'OMBE kama zawadi ya jumla.


Diwani Msollah amemshukuru mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Buyuni Ndg mwenda kwa kuandaa na kufanikisha bonanza hilo,ambalo limefanikiwa kwa kiwango kikubwa 


Sambamba na hilo diwani huyo ameahidi kutoa zawadi ya jezi jozi mbili kwa kila timu zilizoshiriki bonanza hilo ambazo ni Dailema na kitaa, huku pia akitoa pesa taslimu kiasi Cha laki Moja kwa kila timu kama mchango wake wa kukuza mchezo huo wa chandimu.
Amesema kitendo cha kuamua kushiriki michezo ni jambo kubwa na la mfano wengine kwani michezo ni maono, hivyo amewaasa vijana wa kata ya buyuni kulinda na kudumisha amani ya nchi kwani taifa linawategemea vijana hivyo amewasihi vijana kuilinda nchi yao kwani hakuna nchi nyingine hivyo wailinde kwa ghalama yoyote Ile amesema mh Diwani Jesca.
Naye mwenyekiti wa Mtaa wa Buyuni Bw. Sylanus Benard mwenda amemshukuru Diwani huyo kwa kitendo chake Cha kuchangia msaada wa jezi na pesa taslimu kwa timu ya dailema, jambo ambalo limwapa faraja kwa kuendelea kuandaa matamasha na mabonanza ya michezo mengine yenye lengo la kulinda maadili ya vijana kwa ujumla, na kutunza Amani nchini.












 



















Powered by Blogger.