NCHI ZA AFRIKA ZAHIMIZWA KUSHIRIKIANA KATIKA KUIMARISHA MATUMIZI BORA YA NISHATI
*📌Tanzania Yapiga Hatua Kubwa Katika Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia*
*📌Ushirikiano wa Serikali, Sekta Binafsi na Washirika wa Maendeleo Wawekewa Mkazo*
Mhe.Ndejembi ametoa wito huo leo Desemba 10, 2025 wakati akihutubia Kongamano la Nishati la Umoja wa Nchi za Afrika (AU) katika Makao Makuu ya Umoja huo Addis Ababa nchini Ethiopia.
Nchi za Afrika zinapokutana hapa kama wadau wa sekta ya Nishati ni lazima tuungane kwa pamoja katika kutekeleza mipango yetu kwa ajili ya Afrika yetu kwani Serikali ya Tanzania ipo tayari kufanya kazi na Sekta Binafsi, Washirika wa Maendeleo na Wadau wote katika kuhakikisha tunapiga hatua kubwa ya kiuchumi na kijamii," Amesema Mhe Ndejembi.
Aidha Mhe Waziri Ndejembi ameshiriki mjadala wa Mawaziri wa Nishati wa Nchi za Afrika ambapo alitoa taarifa ya hatua kubwa iliyopigwa na Tanzania katika kusimamia ufanisi wa Nishati pamoja na matumizi ya Nishati safi ya kupikia
Mhe. Ndejembi ameeleza kuwa Tanzania tayari imeshazindua na kutekeleza mkakati wa Taifa wa miaka 10 wa matumizi ya Nishati safi ya kupikia (2024-2034), sambamba na mkakati wa Mawasiliano na kuandaa mpango kazi wa kutekeleza mikakati hiyo ili kuufikia umma wa Watanzania
Katika ziara hiyo Mhe Waziri Ndejembi ameambatana na Kamishna wa Umeme na Nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga.






Post a Comment