KANISA LISIHUSISHWE NA CHAMA CHA SIASA:MWL LUDOVIC
Desemba, 30 2025
Dar es salaam
Jamii imeaswa kutofungamanisha kanisa katoliki na chama au vyama vya siasa na kuwa kanisa sio msemaji wa siasa au taasisi yoyote kisiasa, kwa kuwa so lengo la dini ya kiklisto.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Disemba 30,2025 jijini Dar es Salaam, muumini wa Kanisa Katoliki, Mwalimu Ludovick Joseph amesema ametoa maoni yake kama muumini aliyebatizwa na anayepokea sakramenti, kwa nia ya kulinda umoja, maadili na heshima ya Kanisa Katoliki, huku akisisitiza kuwa tafakari hiyo haitokani na chuki wala uasi.Mjadala huu unatokana na imani kwamba, pamoja na kanisa kuanzishwa na Kristo, viongozi wake ni wanadamu wenye mipaka na wanaoweza kukosea, hivyo wanapaswa kuongozwa na Injili, unyenyekevu na mfano wa Kristo mchungaji mwema”,Amesema.
Akinukuu Sheria ya Kanisa (Canon Law), amesema waumini wanatambuliwa kisheria kuwa na haki ya kutoa maoni, ushauri na malalamiko yao kwa wachungaji wa kanisa kuhusu masuala yanayolihusu kanisa huku akibainisha kuwa hatua hiyo si uasi wala dhambi inapofanyika kwa kuzingatia misingi ya kanisa.
Katika tafakari yake, Joseph amekemea matumizi ya madhabahu kama majukwaa ya siasa au lugha za matusi, akisisitiza kuwa mahubiri ya Kikatoliki yanapaswa kubaki kuwa chombo cha kufundisha Injili na kuimarisha imani ya waumini.



Post a Comment