SERIKALI KUONDOA UBAGUZI, KUHIMARISHA MIUNDOMBINU,UNGUJA NA PEMBA
Amesema katika kufanikisha malengo hayo, Serikali itawawezesha wananchi kwa kuwapatia mikopo isiyo na riba, mafunzo ya ujasiriamali, na kuendeleza maeneo ya michezo ili kuwawezesha kujikimu na kuinuka kiuchumi.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 06 Oktoba 2025 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwale, Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika mwendelezo wa kampeni zake kisiwani humo.
Rais Dkt. Mwinyi amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea na dhamira ya kukifanya Kijiji cha Kwale kuendelea kuwa ngome ya chama hicho, kuakisi historia yake ndefu ya kisiasa.Aidha, Dkt. Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwaomba kura wakaazi wa Kwale na kuwasihi kukichagua Chama Cha Mapinduzi ili kiendelee kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
Akizungumza kwa niaba ya wakaazi wa Kwale, Mzee Shaame Khatibu Hamadi amemshukuru Dkt. Mwinyi kwa juhudi zake za kuendeleza amani na umoja wa Wazanzibari, na kumtia moyo kuendelea kudumisha hali hiyo ya amani na maendeleo kwa ujumla.Wakati huo huo, Rais Dkt. Mwinyi ameshiriki mahojiano ya moja kwa moja kupitia Redio Jamii ya Micheweni, ambapo ameelezea mwelekeo wa kampeni zake na malengo ya uongozi wake katika awamu ijayo endapo atapata ridhaa ya wananchi katika Uchaguzi Mkuu ujao, sambamba na kuwaomba kura wananchi wa Zanzibar.
Post a Comment