𝘿𝙠𝙩. 𝙎𝙖𝙢𝙞𝙖 𝙠𝙪𝙟𝙚𝙣𝙜𝙖 𝙪𝙬𝙖𝙣𝙟𝙖 𝙬𝙖 𝙣𝙙𝙚𝙜𝙚 𝙬𝙖 𝙠𝙞𝙨𝙖𝙨𝙖 𝙆𝙖𝙜𝙚𝙧𝙖


Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻, amesema katika kipindi cha miaka 5 ijayo akipewa ridhaa Serikali yake itaanza ujenzi wa uwanja wa ndege eneo la Kyabajwa katika wilaya ya Misenyi, mkoani Kagera ambao utakuwa na uwezo wa kuhudumia ndege kubwa ikiwemo ndege za abiria zenye uwezo wa kubeba abiria 180 mpaka abiria 220 kutoka maeneo mbalimbali nje ya Kagera.

Amesisitiza kuwa mradi huo ni sehemu ya juhudi za serikali za kuimarisha miundombinu ya usafiri na kusukuma mbele sera ya kilimo biashara, kwa kuwezesha usafirishaji wa mazao na bidhaa za kibiashara kwenda ndani na nje ya nchi.

Dkt. Samia amesema kuwa uwanja huo mkubwa na wa kisasa unatarajiwa kufungua fursa mpya za uwekezaji na kukuza sekta ya utalii, biashara na kilimo ndani ya mkoa wa Kagera na maeneo jirani.

Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Kyaka wilayani Misenyi, Dkt. Samia amesema;

“Tumeanza kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa katika eneo la Kyabajwa."

"Awali, ilipendekezwa Omukajunguti, lakini eneo hilo halikufaulu vizuri katika upembuzi yakinifu, hivyo tumeamua kujenga Kyabajwa."

Aidha, Amebainisha kuwa uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuhudumia ndege kubwa za kimataifa kama Boeing 737-900, zenye uwezo wa kubeba abiria 180 hadi 220, jambo litakalofungua milango ya kiuchumi na fursa za biashara kwa wananchi wa Missenyi na maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Uganda.

Powered by Blogger.