WAZAZI WALIMU WA MADRASA DUMISHENI USHIRIKIANO KWA AJILI YA WATOTO WETU: MAKAMO HEMED ABDULLAH

Na Mwandishi wetu 

3.09.2025

Zanzibar 

Wazazi na walezi wametakiwa kushirikiana na walimu wa madrasa katika kuwaendeleza vijana wao kwenye mambo ya khairat ikiwemo kusoma maulidi na kumtukuza mtume muhamadi ( S.A.W) 

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla katika maadhimisho ya Maulid ya kuzaliwa kwa mtume Muhammad (S.A.WA ) Mwezi 11 Mfungo sita mwaka 1447 Hijjiria yaliyoyanyika katika Kiwanja cha Polisi Madungu Chake Chake Pemba.

Amesema kuwalea vijana katika malezi bora yenye kufuata mafundisho yaliyomo ndani ya kitabu kitakatifu cha Qur-an pamoja na kuwafundisha mambo mema ikiwemo kusoma maulidi kutapelekea kupata kizazi chema chenye kumcha Mwenyezimungu na kumtukuzaa mtume Muhammad ( s.a.w ).

Alhajj Hemed amefahamisha kuwa ni lazima walimu wa madrasa kuhakikisha wanaendeleza kusoma maulid kila ifikapo mfungo sita ili kuendelea kudumisha mila na silka za kiislamu pamoja na kuwafunua vijana kama walivyofanya wanazuoni waliopita kabla yao

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka watu wenye uwezo kuwasaidia walimu wa madrasa katika kufanya maulid kila ifikapo mfungo sita jambo ambalo linapelekea kuzidisha upendo na mshikamano baina yao

Sambamba na hayo Alhajj Hemed amewasisitiza waumini wa dini ya kiislam na wazanzibar kwa ujumla kuendelea kuitunza  amani na utulivu uliopo nchini unaopelekea kufanya harakati mbali mbali za kidini na kimaendeleo ikiwemo kukusanyika kusoma maulid na kumswalia Mtume Muhammad (S.A.W).

Aidha makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewasisistiza wananchi wa Pemba kutokubali kutumiwa vibaya na wanasiasa kwa maslahi yao binafsi na kutokuitakia mema Zanzibar
Kwa upande wake katibu mtendaji ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. KHALID ALI MFAUME amesema kuwa ofisi ya Mufti wa Zanzibar itaendelea kuratibu na kusimamia shughuli zote za kidini ikiewemo kuadhimisha kuzaliwa kwa mtume Muhammad ( S.A.W ) kwa kusoma maulid kila ifikapo mfungoo sita.

Sheikh Mfaume amewataka waumini wa dini ya kiislamu na walimu wa madrasa kuwa wamoja na kudumisha mapenzi baina yao ili kuendana na sifa alizokuwa nazo mtume Muhammad ( S.A.W ).


 

Powered by Blogger.