WATANZANIA WAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 29.
Na Moshi saidi.
Mjumbe wa kamati ya ushindi ya chama cha Mapinduzi ccm (UWT) Taifa nyanda za juu kusini ambaye pia ni Mbunge Mstaafu Mhe.Sophia Mwakagenda amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa oktoba 29 2025.
Mwakagenda amesema ni vyema watanzania wakajitokeza kutumia demokrasia yao katika kuwachagua Viongozi makini wa chama hicho cha Mapinduzi kwa nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani watakaowaletea maendeleo kwa miaka mitano ijayo.
Amesema ccm ina mgombea makini ambaye Dkt.samia suluhu Hassan anatosha kuendelea kuaminiwa na wananchi kulingana na kazi kubwa aliyoifanya kwa kipindi cha miaka 4 ya uongozi wake kwakuwa ana sifa na anastahili kupewa nafasi hiyo.
"Nawaomba watanzania wenzangu tujitokeze kwa wingi katika uchaguzi huu wa oktoba ili tufanye maamuzi sahihi ya kumchagua Dkt.Samia wabunge pamoja na madiwani wetu wa ccm ili watuletee Mambo ya mazuri ya kimaendeleo kwa Taifa letu" amesema Mwakagenda.
Mwakagenda ameongeza kuwa serikali ya Rais Dkt.samia na chama cha ccm ni ipo makini katika kuwajali na kuwathamini Watanzia wote hivyo wameendelea kushauriwa kutofanya makosa katika kumpigia kura nyingi za ndio ili aweze kulipeleka mbele gurudumu la kimaendeleo hususani katika kuiendeleza miradi mbalimbali ya kimkakati kama alivyoiendeleza kutoka kwa mrithi wake hayati Dkt.John Pombe Magufuli.
Wajumbe hao wa ccm UWT nyanda hizo za juu kusini wanaendelea na uhamasishaji wa kutafuta kura kupitia mikutano mbalimbali ya kampeni katika mikoa ya Njombe Songwe na Mbeya ili kukipa ushindi chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Post a Comment