KWENYE ELIMU WANA KINONDONI HAWAMDAI RAIS DKT SAMIA: TARIMBA
Septemba 13 2025
Dar es salaam
Mgombea mbunge wa Jimbo la Kinondoni
TARIMBA Abass Gulam, amesema katika
uongozi miaka mitano ya Rais Dkt Samia
suluhu hassan amekamilisha MIRADI yote
ya elimu katika jimbo la Kinondoni.
Ameyasema hayo Leo hii Septemba 13 2025, kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni kwa Jimbo la Kinondoni uliofanyika kwenye viwanja vya CCM Mwinyijuma mwanyamalaAwali mgeni rasmi kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa jumuiya ya WAZAZI taifa Mhe Ali salum Hapi amesema chama Cha Mapinduzi kimemteuwa mgombea Abas tarimba kwa kuwa kinatambua mchango na kazi aliyoifanya wakati wa uongozi wake kwenye muhula wake wa kwanza
Tarimba ambaye anawania UBUNGE kwa muhula wa pili amesema amekishukuru chama Cha Mapinduzi kwa kumuamini na kumteuea kuwa mgombea kwa tiketi ya chama hicho pili ameahidi wananchi wa Jimbo la Kinondoni KUENDELEZA Yale yote waliyoyaanza katika kipindi Cha kwanza
Naye mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM kwa Jimbo la Ukonga mheshimiwa Jerry slaa amewataka wakazi na wananchi wa Kinondoni kumpigia kura mh TARIMBA pamoja na mgombea urais kwa tiketi ya CCM Mhe Dkt Samia suluhu hassan kwenye nafasi ya urais
Uchaguzi mkuu umepangwa kufanyika Oktoba 29 Mwaka huu ambapo jumla ya vyama 17 vikitataraji kushiriki uchaguzi huo
Post a Comment