DKT. BITEKO AHIMIZA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO VIKAO VYA KIMKAKATI VYA WENYEVITI WA BODI

Awakumbusha kuhusu dhamana waliyobeba ya kubadili maisha ya watanzania kupitia mtaji wa shilingi Trilioni 86 waliopewa*

📌 *Afunga Kikao kazi cha Tatu cha Wenyeviti wa Bodi, Wakuu wa Taasisi*

📌 *Asema Rais, Dkt. Samia anatambua mchango wa Taasisi za umma; ana matarajio makubwa kutoka kwao*

📌 *Awakumbusha kutekeleza Maagizo yaliyotolewa na Makamu wa Rais*

📌 *Kikao kazi chafanyika kwa mafanikio; chahusisha washiriki zaidi ya 600*

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko  amewahimiza Wenyeviti na Wakuu wa  Taasisi za Umma nchini kusimamia utekelezaji wa maazimio ya kimkakati yanayofikiwa katika vikao kazi wanavyofanya kwa kutambua kuwa wamebeba dhamana ya kuboresha maisha ya Watanzania kupitia mtaji wa shilingi Trilioni 86 ambao Serikali imewekeza kwenye Taasisi na mashirika yake.

Dkt. Biteko ameyasema hayo tarehe 26 Agosti 2025 jijini Arusha wakati akifunga kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (CEOs FORUM 2025).

 “Watanzania wanawategemea ninyi 

kuwabadilishia maisha, kama tunazungumza kuhusu umaskini wa watu, Serikali inapaswa kuwa kiongozi wa kuwaondolea watu umaskini wao, hivyo hamna budi kutambua  kuwa mnalo deni la 

kuboresha hali zetu na maisha yetu.” Amesema Dkt. Biteko

Dkt. Biteko amewahakikishia Watendaji hao kuwa Serikali katika ngazi zote inatambua mchango wa taasisi 

na mashirika katika ukuaji wa uchumi na pia inatambua mchango wa vikao kazi vya watendaji hao ambavyo vimepelekea mashirika kuongeza mchango wake katika mfuko mkuu wa Taifa.

" Vikao kazi hivi mnavyofanya vimeonesha mchango wake katika uchumi, mfano katika kikao kazi cha mwaka 2024 mliazimia mashirika ya umma yaboreshe utendaji na  kuongeza uchangiaji katika mfuko mkuu wa Serikali na  matokeo yameonekana mfano Shirika la Maendeleo ya Petroli ( TPDC) liliongeza uchangiaji wake kwa asilimia 100, shirika hili liliongeza uchangiaji wake kutoka shilingi bilioni 5.5 kwa mwaka 2023/2024 hadi shilingi bilioni 11.1 mwaka 2024/2025." Amesema Dkt.Biteko



 

Powered by Blogger.