AHADI YA SERIKALI KUFIKISHA UMEME WA GRIDI KAGERA YATEKELEZWA

Ahadi ya Serikali ya kufikisha umeme wa gridi ya taifa katika Wilaya zote za Mkoa wa Kagera imetekelezwa baada ya Serikali kusaini mikataba ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Benako, Ngara  hadi Kyaka  wilayani Misenyi na kituo cha kupoza umeme cha Benako cha msongo wa kilovoti 220/33, hatua inayotoa uhakika kwa Mkoa huo sasa kupata umeme wa gridi badala ya kutegemea umeme kutoka Uganda kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini kwa mikataba hiyo jijini Dodoma tarehe 25 Agosti, 2025, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa kuanza kutekelezwa kwa mradi huo ni moja ya maelekezo ya Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa na kiu ya kutekeleza ahadi ya Serikali kwa wananchi wa Kagera  ya kupata umeme wa uhakika muda wote ili kutekeleza shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Kupitia mradi huu, Mkoa wa Kagera kwa mara ya kwanza na wenyewe unaingia kwenye gridi ya Taifa hasa na hivyo kuongeza uhakika wa upatikanaji wa umeme hususan katika Wilaya za Bukoba, Muleba, Misenyi, Karagwe, Kyerwa  na maeneo mengine ya jirani, nawahakikishia watu wa Kagera kuwa Serikali imeshaamua mradi  huu ufanyike kwa wakati kwa  miezi 24 tu" Amesema Dkt. Biteko

Dkt. Biteko amesema, Kagera ambayo mahitaji yake ya umeme hayazidi megawati 47 baada ya muda itakuwa na uhakika mkubwa wa upatikanaji umeme kwani kutakuwa na njia mbalimbali za kufikisha  umeme mkoani humo ikiwemo Benako- Karagwe hadi Kayaka,  Nyakanazi- Biharamulo hadi Muleba na kuna mradi mwingine mkubwa  unaotarajiwa kujengwa kutoka Ibadakuli hadi Mbarara Uganda wa kV 400. Vilevile kuna mradi wa uzalishaji umeme wa Kakono wa megawati 87 ambao upo katika hatua za mwisho za kutafuta Mkandarasi.

Dkt. Biteko amesema, Kagera ambayo mahitaji yake ya umeme hayazidi megawati 47 baada ya muda itakuwa na uhakika mkubwa wa upatikanaji umeme kwani kutakuwa na njia mbalimbali za kufikisha  umeme mkoani humo ikiwemo Benako- Karagwe hadi Kayaka,  Nyakanazi- Biharamulo hadi Muleba na kuna mradi mwingine mkubwa  unaotarajiwa kujengwa kutoka Ibadakuli hadi Mbarara Uganda wa kV 400. Vilevile kuna mradi wa uzalishaji umeme wa Kakono wa megawati 87 ambao upo katika hatua za mwisho za kutafuta Mkandarasi
Ameongeza kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan pia anaendelea kutekeleza miradi mingine ya umeme katika maeneo mengine ikiwemo mradi wa usafirishaji umeme wa kV 400 wa Tanzania- Zambia, mradi wa Usafirishaji umeme wa kV 400 Chalinze-Dodoma , mradi wa usafirishaji umeme wa Mkuranga -Pwani ambao utapeleka  umeme kwa wananchi wa Kusini, pia mradi wa usafirishaji umeme wa gridi imara wa Tunduru- Masasi- Mahumbika ambao pia unaenda kutoa uhakika wa umeme katika mikoa ya Kusini
Utekelezaji wa miradi hii yote ya umeme ni kielelezo kuwa, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshaonesha njia ya kuwafikishia wananchi umeme wa uhakika sasa kinachohitajika kwa watendaji ni kukimbia badala ya kutembea kwani kinachotakiwa ni matokeo na siyo kusema sana." Amesisitiza Dkt. Biteko

 

Powered by Blogger.