KOMBOZA: AJITOSA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI

Na Jumanne Magazi 

02.07.2025 

Dar es salaam 

HatamyeMwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Walemavu Tanzania, Hamadi Abdallah Komboza, amepata msukumo mkubwa kutoka kwa viongozi wenzake pamoja na baadhi ya wanachama, wakimtaka achukue fomu ya kuwania Ubunge katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Mbali na msukumo huo kutoka kwa wanaomuamini na kumuunga mkono, Komboza anatekeleza pia wajibu wake wa kikatiba kama raia mwenye sifa stahiki ya kushiriki katika uchaguzi kwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Kwa kuzingatia misingi hiyo, Komboza amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili aweze kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kinondoni katika uchaguzi ujao.
Aidha komboza amesema ni muda kwa upande wake kuingia kwenye kinyanyiro hicho kwani nguvu moyo na hali ya kufanya hivyo anayo, hivyo amekiomba chama chake ikiwapendeza kumteua ili kuweza kumsaidia mh Rais ambaye pia niwenyeki wa chama hicho, DKT Samia suluhu Hassan 
Zaidi ya Wanachama na makada wa chama Cha mapunduzi 105, wamejitokeza kuwania nafasi za kuteuliwa kwenye kinyanyiro Cha uchaguzi mkuu ujao,kwa nyakati tofauti ikiwemo Ubunge,Udiwani kote nchini 

Zoezi ambalo limefika tamati hii Leo Julai 2 2025, ambapo lilianza rasmi juni 28 mwaka huu kwa wanachama WA CCM kujitokeza kuchukua FOMU na kurudisha  Tayari kuomba kuteuliwa na chama kupeperusha bendera ya chama hicho.


 

Powered by Blogger.