TANZANIA NA DR CONGO KUENDELEZA USHIRIKIANO WA KIMKAKATI KUJADILI KONDOA GHARAMA ZA VIZA
Na Jumanne Magazi
16.06.2025
Dar es salaam
Kamishna wa idara ya uhamiaji, Dkt Anna Makakala amesema tanzania na jamhuri ya demokrasia ya congo wanampango wa uhusiano wa kimkakati kuhusiana na maswala ya uhamiaji hususani katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu.
Akizungumza nje ukumbi wa Mkutano maalum baina ya Maafisa wa ngazi za juu idara ya uhamiaji wa nchi zote mbili amesema tanzania na congo zimekuwa na uhusiano wa lol ndugu baiana ya wananchi wa pande zote mbili hivyo kumekuwa na mijadala mungu juu ya ushirikiano wa pamoja.Katika kuthamini na kuendeleza uhusiano huu, Tanzania imeendelea kuwa makazi salama kwa raia wa DRC katika nyakati zote.
Aidha Makakala amesema Mkutano tunaoufanya leo unalenga, pamoja na mambo mengine, kujadili namna bora ya kuimarisha ushirikiano katika kusimamia uhamaji kati ya nchi zetu mbili.
Ni kwa muktadha huo tunatoa msisitizo mkubwa juu ya suala la msamaha wa visa kwa raia wa DRC na kurudisha fadhila hiyo kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Suala hili linapaswa kupata suluhisho la kudumu kwa kuzingatia madhumuni ya Itifaki ya Soko la Pamoja ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa uhamiaji nchini demokrasia ya congo, Roland Kashantwale amesema mazungumzo yanayofanyika Leo yanalengo la kuwapa unafuu raia wa nchi hizi mbili katika maswala ya maingiliani ikiweo shughuli za KIUCHUMI kisiasa na kiutamaduni hivyo ni muda sasa kwa mataifa haya kukaa kama HIVI kutatua na kupanga mipango endelevu kwa maslahi ya mataifa haya mawili.
" Ni kweli tumekaa na mwenzangu kamishina Ana Makakala tumeonelea kuwepo kwa ajenda muhimu ikiwemo maswala ya visa ambapo tunachukuwa maoni ya pande zote mbili Kisha tupeleke kwa viongozi wakuu wa nchi hizi mbili ili nao waon namba ya kuliendea jambo hili amesema Roland"
Mbali na mambo mengine mkurugenzi huyo amemshukuru Rais wa Tanzania DKT Samia suluhu Hassan kwa juhudi zake ambazo "sisi kama wakongo tunaona muelekeo mzuri kwa watu wetu amemaliza kusema mkurugenzi huyo"
Tanzania imekuwa ikifanya mikutano ya mara kwa mara na viongozi wa nchi zote Wanachama wa jumuiya za nchi za Afrika mashariki katika maswala ya uhamiaji ili kuweka utaratibu rafiki kwa maslahi mapana ya nchi Wanachama.
Post a Comment